Friday, November 11, 2011

NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA SIDO YA NYANDA ZA JUU KUSINI MKOANI RUKWA

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu (MB) akikata utepe kama ishara ya kufungua rasmi maonyesho ya 9 ya SIDO ya nyanda za juu kusini inayoshirikisha mikoa ya Rukwa, Iringa na Mbeya. Kulia kwake anayeshuhudia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana. Maonyesho hayo yanafanyika katika Uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa  kwa kushirikisha wajasiriamali kutoka zaidi ya mikoa 14 nchini na wengine kutoka nchi jirani za Kenya na Burundi.


Naibu Waziri akisalimiana na Meneja wa SIDO Mkoa wa Rukwa ambao ndio wenyeji Ndugu Martin Chang'a mara baada ya kuwaili katika uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa kwa ajili ya kuzindua rasmi maonesho hayo. Kwa mujibu wa Meneja huyo wa SIDO maonyesho hayo yatadumu kwa mda wa siku 6 kuuanzi tarehe 9-14 ambapo ndio itakuwa kilele na atakefunga maonesho hayo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.  

Mkurugenzi Mkuu wa SIDO nchini Ndugu Mike Laizer akifafanua jambo kwa Naibu wa Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu kwenye banda la SIDO. Kulia kwa Naibu Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana.

Naibu Waziri akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joyce Mgana akimpokea na kumkaribisha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga.

Wajasiriamali wa Rukwa wakinadi bidhaa zao za Asali na Nta. Asali inayopatikana Mkoani Rukwa ni asali yenye ubora mkubwa (Grade One), kwa wale watakaopata bahari ya kutembelea maonyesho haya wanaweza kujipatia bidhaa hiyo na nyinginezo nyingi. 

Uhifadhi wa Mazingira nao umepewa kipaumbele Mkoani Rukwa, Mjasiriamali wa uhifadhi wa Mazingira wa kikundi cha REYO akinadi miti aina mbalimbali inayofaa kwa uhifadhi wa mazingira na matumizi mengineyo katika maonesho hayo.

Mjasiriamali Mama Grace Masawe kutoka Arusha anayejishughulisha na kazi za mikono akionyesha cheti alichozawadiwa kama Mjasiriamali mwenye banda bora katika maonesho hayo, alikabidhiwa Cheti hicho na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Lazaro Nyarandu. Mama Grace Mkurugenzi Mtendaji wa Masawe Curio and Crafts kutoka Arusha.

Maonyesho hayo yakiendelea

Tiba asilia pia zinapatikana katika maonyesho hayo

Kaimu Katibu wa Mkuu wa Mkoa Ndg. Frank Mateny kushoto, Makatibu Tawala Wasaidizi  Ndugu Samson Mashalla Utawala,  Ndugu Sebastian J. Mundia Menejimenti ya Serikali za Mitaa na Ndugu Willy Mzava Uchumi na Uwezeshaji wakisubiri kumuaga Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara katika Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga

Utamaduni wa Kimasai nao unapatikana katika maonesho hayo

Meneja wa SIDO Mkoa wa Rukwa kulia Ndugu  Martin Augustino Chang'a pamoja Katibu wa Mkuu wa Mkoa Rukwa Ndugu Frank Mateny wakisubiri kumuaga Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara katika Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga.

Haya mambo ya ajabu pia yapo, inadaiwa ni Mtu wa ajabu kutoka Burundi aliyezaliwa kichwa kitupu, ana uwezo wa kuzungumza lugha tofauti na wakati wa kumuhoji alidai kuwa chakula chake ni Sindano maalum. Katika akili ya kawaida haifikiriki na wengi wa watu waliomtembelea huyu bwana ikiwa ni pamoja na mimi walisema haya ni MAZINGAUBWE. Huyu bwana anapatikana kwenye banda moja na ili kuweza kumuona inatakiwa kulipia shillingi mia tano tu. Nilishuhudia baadhi ya watoto waliopata bahati ya kumuona wakilia kwa hofu na wengine wakiwa na mshangao mkubwa.

Vikundi vya ngoma vilikuwepo kutoa burudani

Mjasiriamali wa Rukwa anayejishughulisha na utengenezaji wa viatu kwa kutumia ngozi mbalimbali. Chipawas Leather Tunning wanapatikana maeneo ya Jangwani Wilayani Sumbawanga, wapo pia kwenye maonesho hayo. 

1 comment:

  1. Nawashukuru sana wajasiriamali wa Rukwa na wengine ambao wamejitokeza kwenye maonyesho ya SIDO Sumbawanga kuonyesha ubunifu wao na jitihada zao za kujikwamua kiuchumi.Hii ni nafasi ya kuonekana na kujitambulisha kwenye mtandao wa masoko ndani ya nchi na kwingineko duniani.
    Nawatakia mafanikio mema katika maonesho

    George Nkwera
    Sumbawanga - kwa sasa UK

    ReplyDelete