Monday, November 28, 2011

WAKE WA VIONGOZI WAKUU WA SERIKALI WATEMBELEA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MTANZANIA LINALOWAKILISHWA NA JAMII ZA WANARUKWA NA KATAVI KATIKA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO

Mama Zakia Gharib Bilal, Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB) wakati alipowasili kutembelea Tamasha la Mtanzania lililowakilishwa na Jamii za WanaRukwa na Katavi katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Katika msafara mwenyekiti alikuwa Mama Zakia Bilal akiongozana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda, Mke wa Makamu wa Pili wa Zanzibar Mama Asha Seif Ali Iddi, Mlimbwende wa Tanzania mwaka 2011 (Miss Vodacom 2011) Salha Israel na Wake wa mawaziri mbalimbali.

Katika ziara yao hiyo walipata kujionea mambo mbalimbali ya utamaduni wa MwanaRukwa na Katavi yakiwemo vyakula vya asili, vifaa vya kutengenezea chuma, silaha za jadi na tiba asilia.

Kutoka kushoto ni Mama Asha Seif Ali Iddi Mke wa Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mama Tunu Pinda Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mama Zakia Gharib Billal Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mzee Zeno Nkoswe ambaye ndiye mwenyeji wa sherehe hizo kimila. Nyuma ya Mzee Nkoswe ni Miss Tanzania 2011 Salha Israel wakijitambulisha kwa kwenye tamasha hilo.

Mama Zakia Gharib Billal (katikati) na Mama Tunu Pinda wakionyeshwa aina ya udongo maalum uliokuwa ukitumika katika kutengenezea chuma. Jamii za WanaRukwa na Katavi zilikuwa na Teknolojia ya kuyeyusha na kutenegeneza chuma.
Kikundi cha Uyeye kutoka Mpanda kikitoa burudani. Kikundi hiki kinasifika kwa kucheza na nyoka. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Manyanya, Chifu Kayamba wa Inyonga na Miss Tanzania 2011 Salha Israel.
 
Ilungu ni aina ya mtambo uliokuwa ukitumika na Jamii za WanaRukwa katika harakati zao za kutengeneza Chuma. Mtambo huo ulikuwa ukiyeyusha udongo maalum na baadae kuundwa chuma kamili. Mtambo huo umejengwa katika Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama ili kuhifadhi kumbukumbu na Tamaduni za Mtanzania. 

No comments:

Post a Comment