Thursday, December 22, 2011

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO LA SUMBAWANGA MJINI AKABIDHI KADI YA UANACHAMA NA KUJIUNGA NA CCM

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Rukwa Mhe. Hiporatus Matete akionyesha kadi ya CHADEMA aliyokabidhiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho katika Manispaa ya Sumbawanga Ndugu Geophrey Shayo (kulia) katika ukumbi wa Sabasaba uliopo katika Manispaa ya Sumbawanga. Anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum CCM wa Mkoa wa Songea ambaye ni Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya. Mwenyekiti huyo amechukua hatua hiyo kwa madai kuwa amechoshwa na udanganyifu ambao upo ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini Mhe. Aeshi Hillal (kulia) akimpa Ndugu Shayo mkono wa pongezi mara baada ya hatua yake aliyoichukua ya kukabidhi kadi ya CHADEMA kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa na hatimaye kujiunga na Chama hicho. Ndugu Shayo amempongeza Mhe. Aeshi kwa kazi nzuri aliyokwisha kuifanya katika jimbo lake la Sumbawanga Mjini na kusema kuwa hatua yake hiyo ya kuihama CHADEMA ni kuja kumpa nguvu ili maendeleo yaweze kuja kwa kasi zaidi katika jimbo hilo. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mhe. Sabas Katepa. 

No comments:

Post a Comment