Thursday, December 8, 2011

MAMA ANNA MKAPA AVUTIWA NA BANDA LA RUKWA KWENYE MAONESHO YA MIAKA 50 YA UHURU KATIKA VIWANJA VYA MWL. J.K. NYERERE DSM ZAMANI SABASABA

Mhe. Mama Anna Mkapa Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akikaribishwa katika Banda la Rukwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe katika Jengo la Mama Anna Mkapa lililopo katika Viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere yanapofanyikia maonesho ya sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Miongoni mwa mambo yaliyomvutia sana katika banda hili ni Samaki wa Mapambo wanaopatikana katika Ziwa Tanganyika hususan maeneo ya Kipili, Karema na Kasanga.

Mhe. Mama Anna Mkapa aikisaini Kitabu cha wageni katika Banda la Rukwa.

Mama Anna Mkapa akipata maelezo kuhusu rasilimali zinazopatikana Mkoani Rukwa wakiwemo Samaki wazuri kwa Lishe waitwao Mgebuka kutoka Ziwa Tanganyika. Anayeonekana kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt. Rajab Rutengwe na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima (katikati).


Utawala Bora ni Injini Kuu inayosukuma gurudumu la maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. Viongozi pamoja na wataalamu katika banda la Rukwa wakitoa maelezo kwa Mhe. Mama Anna Mkapa jinsi Mkoa ulivyojipanga na kupiga hatua katika sekta ya Utawala Bora katika kipindi chote cha Miaka 50 ya Uhuru.

Mhe. Mama Anna Mkapa akionekana mwenye furaha baada ya kutembelea vibanda vyote vya Rukwa.

Wataalam katika Banda la huduma za jamii kwenye Banda la Rukwa wakiwa wamejipanga kutoa huduma kwa wateja.


No comments:

Post a Comment