Saturday, December 3, 2011

MAONYESHO YA MIAKA 50 YA UHURU MKOA WA RUKWA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Shein alipotembelea banda la Rukwa mara baada ya kufungua maonyesho ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miaka 50 ya Uhuru kutoka Mkoani Rukwa Ndugu Salum Shillingi.

Mkoa wa Rukwa umepewa vibanda sita (6) katika Jengo la Mama Anna Mkapa Mkabala na Jengo la Sabasaba. Vyumba hivyo ni kama vinavyoonekana kwenye picha. Banda la kwanza linazungumzia mambo muhimu katika Mkoa kwa ujumla zikiwemo fursa za uwekezaji na malengo ya Mkoa. Mabanda mengine yanaelezea mambo ya Utawala Bora, Huduma za Jamii na Mipango Miji, Sekta ya Uvuvi, Ujasiriamali Mkoa wa Rukwa na Sekta ya Kilimo na Mifugo.

Kwa wale watakaopata fursa ya kutembelea banda la Mkoa wa Rukwa watapata fursa ya kujionea Utajiri uliopo Mkoani Rukwa na Fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana Mkoani huko. Pia watapata bidhaa mbalimbali kutoka Mkoani Rukwa kama vile Asali yenye ubora wa hali ya juu (First Grade) ya nyuki wakubwa na wadogo pamoja na Samaki wazuri kutoka ziwa Tanganyika. Vipo vivutio pia vya Samaki wa Mapambo kutoka Ziwa Tanganyika.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Said Thibit Mwambungu akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mkoa wa Rukwa. Anayeshudia Mtaalam wa Mifumo ya Kompyuta Ndugu Emmanuel Mwandiga.

Mjasiriamali kutoka Rukwa akinadi bidhaa katika banda la Rukwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Miaka 50 ya Uhuru Mkoa wa Rukwa Ndugu Salum Shillingi kushoto, Wajumbe wa Kamati Ndugu Florence Chrisant na Ndugu Hamza Temba wakiwa katika banda la Mkoa wa Rukwa katika kuelezea mafanikio ya Miaka 50 ya Uhuru katika Mkoa wa Rukwa

Mchumi Florence Chrisant (kulia) na Afisa Habari Mkoa wa Rukwa Ndugu Hamza Temba wakibadilishana mawazo namna ya kufanikisha maonyesho hayo.
Wageni mbalimbali wamevutika kutembelea mabanda ya Rukwa. Hao ni wageni kutoka Bukoba Mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment