Wednesday, December 7, 2011

MBUNGE WA SUMBAWANGA MJINI ATEMBELEA BANDA LA RUKWA KWENYE MAONESHO YA MIAKA 50 YA UHURU KATIKA VIWANJA VYA MWL. J.K.NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya CCM Mhe. Aeshi Hillal (kushoto) akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima alipotembelea banda la Rukwa leo kwenye Maonesho ya Miaka 50 ya Uhuru katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam. Hapo wakitoa huduma kwa wateja.

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa akimsainisha kitabu cha wageni mmoja wa wageni waliofika kupata huduma katika banda la Rukwa. Anayeshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Mhe. Aeshi Hillal. Banda la Rukwa limekuwa likipata wageni wengi kutoka Mikoa na maeneo mbalimbali wakitaka kujifunza mambo mbalimbali kutoka katika Mkoa huo.

Mhe. Aeshi alitembelea vibanda vyote Sita (6) vya Mkoa wa Rukwa katika Maonesho hayo na kufarijika kwa yote aliyoyaona na kuahidi kuleta chombo cha Televisheni cha TBC 1 kesho asubuhi kwa ajili ya kutangaza shughuli zinazofanywa na Banda hilo la Rukwa. Miongoni mwa mambo muhimu yanayoonyeshwa na banda la Rukwa ni Mafanikio yaliyopatikana Mkoani Rukwa kwa kipindi cha miaka 50 ya Uhuru pamoja na kuonyesha Fursa za Uwekezaji zinazopatika Mkoani humo.

Mhe. Mbunge akimnong'oneza Muhariri wa Blogu hii Ndugu Hamza Temba juu ya ziara yake fupi nchini Burundi. Alisema kuwa ziara yake hiyo nchini Burundi ilikuwa ya kikazi iliyomfanya ashindwe hata kuhudhuria Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania lililowasilishwa na Jamii za WanaRukwa na Katavi katika kijiji cha Makumbusho tarehe 15-17/11/2011. 

Jambo muhimu na la msingi alioileza blogu hii ni juu ya mafanikio ya ziara yake hiyo kuwa aliapata fursa ya kukutana na baadhi ya Viongozi wa Serikali nchini Burundi akiwepo Meya wa Jiji la Bujumbura pamoja na Wafanyabiashara wakubwa na kuwaeleza juu Fursa zinazopatikana Mkoani Rukwa. Alisema kuwa wote walifarijika na kuonyesha nia ya kutembea na kuwekeza Rukwa. "Nimechukua contact zao na nitakachokifanya ni kuzipeleka kwa Mkuu wa Mkoa ili kuwapa mualiko rasmi wadau hao waweze kuja kutembea Rukwa na kujionea fursa zilizopo" alisema Mhe. Aeshi.

No comments:

Post a Comment