Thursday, December 8, 2011

NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI AZINDUA KITABU CHA MAFANIKIO YA MIAKA 50 YA UHURU MKOA WA RUKWA LEO

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Aggrey Mwanri (MB) akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Kitabu cha Mafanikio ya Miaka 50 ya Uhuru Mkoa wa Rukwa katika banda la Mkoa huo katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere zamani Sabasaba kwenye maonesho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Anayeshudia ni Katibu Tawala Mkoa huo Ndugu Alhaj Salum Mohammed Chima. Vitabu hivyo vinatolewa bure katika Banda la Rukwa lililopo katika viwanja hivyo kwenye Jengo la Mama Anna Mkapa. 

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akimkabidhi Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Aggrey Mwanri Vitabu vya Mafanikio ya Miaka 50 ya Uhuru Mkoa wa Rukwa mara baada ya kuvizindua leo mchana. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Dkt. Rajab Rutegwe.

1 comment:

  1. Good attempt Rukwa, you have shown a good example

    ReplyDelete