Saturday, December 10, 2011

RC RUKWA ATEMBELEA MAONESHO YA MIAKA 50 YA UHURU KATIKA VIWANJA VYA MWL. J. K. NYERERE DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) akisaini kitabu cha wageni katika Banda la Rukwa lililopo katika jengo la Mama Anna Mkapa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mwl. J.K Nyerere zamani Sabasaba yanapofanyika maonesho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa alifurahia hali aliyoikuta katika banda hilo la Rukwa na kutumia mwanya huo kunadi Sera na vivutio vya Mkoa wa Rukwa kwa baadhi ya wateja walitembelea banda hilo. 

Mtaalamu wa Mifugo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Bw. Respitch Maengo akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kitabu cha Mkoa huo cha Mafanikio ya Miaka 50 ya Uhuru. Kitabu hicho kinaelezea Mafanikio yaliyopatakana katika Mkoa wa Rukwa kwa kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru kwa kila sekta. Kitabu hicho kinapatikana bure katika banda hilo na katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.

Aliingia kazini na kutoa maagizo kwa Wataalamu wa Mipango Miji katika banda hilo la Rukwa kwa kuwaagiza kutenga maeneo maalum yasiyopungua hekari tatu kwa kila Wilaya kwa ajili ya Ujenzi wa Vituo vya kuhifadhia mambo ya Utamaduni (Makumbusho) katika kipindi cha mwezi huu wa Desemba kabla ya tamko rasmi la Mhe. Rais la kuanzisha Mkoa mpya wa Katavi.

Miongoni mwa bidhaa zinazopatikana katika Banda la Rukwa ni Samaki wazuri kwa Lishe aina ya Mikebuka kutoka Ziwa Tanganyika. Hapo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa zawadi ya samaki hao kwa watoto waliotembelea banda hilo la Rukwa na wazazi wao. 

Mhe. Eng. Stella Manyanya (MB) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akijaribisha Kata ya kunywea Maji iliyokuwa ikitumika katika kipindi cha nyuma.Wakati huu tunapoadhimisha Mika 50 ya Uhuru vifaa hivyo vimekuwa havitumiki tena kutokana na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

Alitembelea pia banda la Kagera na kujionea hatua kubwa iliyopigwa na Mkoa huo katika kutengeneza kahawa kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum CCM kutoka Mkoa wa Ruvuma alipata fursa ya kutembelea banda la Mkoa huo wa nyumbani na kujionea shughuli mbalimbali katika Banda hilo. Pichani akikabidhi zawadi ya Samaki aina ya Mikebuka kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kupitia kwa Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Ndugu Revocatus Kassimba.

Ziara ya Injinia Stella Manyanya katika viwanja hivi vya maonesho ya Mwl. J.K. Nyerere iliishia hapa katika lango kuu la kuingilia katika Banda la Mama Anna Mkapa. Aliyesimama kushoto kwake ni Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa RUKWA Ndugu Hamza Temba.

No comments:

Post a Comment