Friday, December 2, 2011

WANARUKWA, KATAVI NA WATANI WAO KIKUNDI CHA NGOMA CHA WANGONI WALIPOTEMBELEA MAKUMBUSHO NA NYUMBA YA UTAMADUNI DAR


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng Stella Martin Manyanya (MB) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho Ndugu Jackson Kihiyo wakati walipotembelea Makao Makuu ya Makumbusho ya Taifa na Wanarukwa na Katavi pamoja na kikundi cha Ngoma kutoka Ruvuma.

Wanakikundi wa Kikundi cha Ngoma kutoka Ruvuma wakiongozwa na muimbaji wao Bi. Angelika Gama wakimsikiliza mtaalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni juu ya Mwenge wa Uhuru uliopandishwa Mlima Kilimanjaro Miaka ya 60.

Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Dkt. Paul Msemwa akiwakaribisha Wanajamii wa Rukwa na Katavi walipowasili katika makumbusho hayo, aliyeshikana naye mkono ni Mzee Zeno Nkoswe.

Jamii ya wanaRukwa na Katavi walipata fursa ya kutembelea Makumbusho hayo na kujionea mambo mbalimbali ya kihistoria, hapo wakiangalia magari tofauti yaliyotumiwa na hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere wakati wa uhai wake akiwa madarakani.

Kikundi cha ngoma cha Wangoni kutoka Ruvuma katika picha ya pamoja na Chifu wao aliyeshikilia mtoto, Kikundi hiki cha ngoma kilikuwa sehem ya vikundi vya ngoma vilivyoonyesha ushirikiano mzuri kwenye Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania lililowasilishwa na jamii za wanaRukwa na Katavi.

No comments:

Post a Comment