Thursday, December 22, 2011

WAZIRI MKUU AWASILI WILAYANI MPANDA KWA AJILI YA MAPUMZIKO MAFUPI

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (MB) akiwasili katika uwanja wa ndege wa mpanda tayari kwa kuanza likizo yake fupi itakayoambatana na Skukuu za Krismasi na Mwaka Mpya. Yeye na msafara wake walitokea DRC kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais Kabila mara baada ya kuibuka mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo hivi karibuni.

Mara baada ya kushuka kwenye ndege alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) nakuelekea katika mapumziko mafupi katika chumba cha kupumzikia uwanjani hapo.

Alilakiwa na viongozi wa Chama, Serikali, watumishi pamoja na wananchi wa Mpanda. Pichani akisalimiana na Chifu Kayamba wa Inyonga.

Waziri Mkuu akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakizungumza na Mwanachi aliyekuja kumpokea katika uwanja wa Ndege wa Mpanda. Waziri Mkuu anatarajiwa kukamilisha likizo yake mwanzoni mwa mwezi Januari katika mwaka mpya wa 2012.

No comments:

Post a Comment