Thursday, January 5, 2012

JINAMIZI LAENDELEA KUIKUMBA SHULE YA SEKONDARI LUSAKA, WALIMU WAVAMIWA WATOKEA UHARIBIFU MKUBWA WA MALI

Ofisi ya Mkuu wa Shule hiyo ikiwa imeharibiwa vibaya

 Mkuu wa shule ya sekondari lusaka Jonasio Simsokwe kushoto na Mwalim Joseph Luoga kulia wakielezea mazingira ya tukio hilo la uvamizi na jinsi nyumba zilivyobomolewa kwa mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Bw. Crispin Luanda
  
Afisa Mtendaji Kati ya lusaka Bw. Omelo Mbalazi akifafanua jambo kuhusiana na tukio hilo la uvamizi..kulia kwake ni afisa elimu Emanuel Kipele, mwakilishi wa Mkurugenz Crispin Luanda na Afisa utumishi John Maholani wote kutoka Halamashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.


Waalimu saba wanaofundisha katika shule ya sekondar ya Lusaka iliyopo kata ya lusaka Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa wamevunjiwa nyumba zao pamoja na baadhi ya ofisi katika jengo la utawala, baada ya watu wasiojulikana kuvamia shule hiyo usiku wa manane.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia desemba 27 mwaka jana ambapo wavamizi hao walivunja vioo vya madirisha katika ofisi ya mkuu wa shule hiyo pamoja na nyumba kadhaa za walimu, pamoja na stoo ya shule.

Timu ya wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi ilitembelea shule hiyo na kushuhudia uharibifu uliofanywa na wavamizi hao, ambapo kwa mujibu wa mwakilishi wa mkurugenzi Crispin Luanda  hasara ya uharibifu huo ni zaidi ya shilingi milioni 2.5.

Mbali na kuvunja sehemu kadhaa katika majengo hayo, wavamizi hao pia walivunja stoo ya shule hiyo na kuiba mahindi kiasi cha gunia moja na debe tatu yaliyokuwa yakitumiwa na wanafunzi wa shule hiyo kwa ajli ya chakula.

Kufuatia tukio hilo ambalo limekuwa likijirudia kwa mara kadhaa sasa katika shule hiyo, walimu wa shule hiyo wakiongozwa na mkuu wa shule Jonasio Simsokwe wamemuomba Mkurugenzi wa Wilaya ya Sumbawanga kuwaondoa katika shule hiyo mpaka hali ya usalama itakapoimarishwa ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea.

Na Ramadhan Juma (Afisa Habari-DED Sumbawanga)

1 comment:

  1. yaani ndugu zangu wa hapo lusaka ninawahurumia na tutaendelea kuwa masikini. Inaelekea umuhimu wa elimu amuuoni subilini hao waalimu waondoke arafu watoto wetu wakose hiyo huduma muhimu" NGAMUVIPELE"

    USHAURI WANGU KWA UONGOZI WA MKOA NI KWAMBA WATU WA USALAMA WAKISHIRIKIANA NA POLISI NI RAHISI SANA KUBAINI HAO WAHUNI. HATA MIMI NINGEKUWA JILANI NA HUKO NINGEJITOLEA KUWATAFUTA HAO WAHUNI MAADUI WA MAENDELEO.
    POLISI JAMII "COMMUNITY POLISI"ITAMIKE PIA KATIKA KUWABAINI HAO WAPINGA MAENDELEO YA KWETU.

    ReplyDelete