Wednesday, January 11, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA ATOA ZAWADI YA MWAKA MPYA KWA WAFUGWA WA MAHABUSU MKOANI HUMO

Afisa Habari na Mahusiano Mkoa wa Rukwa, Hamza Temba (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Magereza wa Mkoa Rukwa George James Kiria zawadi za mwaka mpya kwa niaba ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya (MB).  Zawadi hizo ni kilo 40 za nyama, debe moja la vitunguu, kilo 5 za nyanya, na sabuni za mche box 5. Zawadi hizo zitatumiwa na wafungwa katika gereza la mahabusu la Manispaa ya Sumbawanga.  

Baadhi ya zawadi zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa huo zikipokelewa na Maofisa wa Magereza Mkoa wa Rukwa. Kulia ni Mwandishi wa habari wa Star TV na RFA Samy Jumaa Kisika.

 Picha ya pamoja kati ya Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Hamza Temba (wa pili kulia) na Ofisa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa George James Kiria wa pili kushoto. Kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa Job Philipo na Mwandishi wa Habari Samy Jumaa Kisika (kushoto).

1 comment:

  1. Habari za kazi mimi huwa ni msomaji ya blog hii na nimeguswa sana na utendaji kazi ya mkuu wa mkoa wa sumbawanga.Huyu Mheshimiwa ni mfano mzuri wa uongozi bora ambao nchi hii inahitaji viongozi wanaongoza kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa.Ushahidi unaonyesha Mkubwa wa serikali akishika ufagio na kufagia barabara na kuingia ndani ya mtaro kuondoa maji machafu, hawa ndio viongozi ambao tunawahitji watuongoze.Mungu akubariki sana mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Sumbawanga.Sisi watanzania wenzako tunatambua jinsi unafanyakazi kwa bidii.WEWE NI MFANO MZURI UNAOFAA KUIGWA.Serikali iangalie viongozi wa aina hii ili kuwapa nafasi nyeti kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

    ReplyDelete