Friday, January 13, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AZINDUA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA MJINI SUMBAWANGA LICHA YA MVUA KUBWA KUNYESHA JANA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati) akifagia kwenye moja ya barabara za Mji wa Sumbawanga Mkoani humo jana katika uzinduzi wa kampeni ya kusafisha Mji huo ijulikanayo kama "SUMBAWANGA NG'ARA 2012". Wanaojumuika naye kwenye usafi huo ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Samwel Simwela. Mkuu huyo wa Mkoa ameanzisha Kampeni hiyo ambayo itakuwa ni ya kudumu baada ya kuona Manispaa hiyo imezorota katika usafi wa mazingira.

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akijumuika na Mkuu wa Mkoa huo katika uzinduzi wa Kampeni hiyo.

Huku Mkuu wa Mkoa huo akiendelea na ufagiaji wa barabara za Mji huo wa Sumbawanga Daladala nazo zilikuwa zikiendelea na shughuli zake za kusafirisha abiria kupitia barabara hizo. Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao.

Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini Mhe. Aeshi Hillal akitoa uchafu kwenye mtaro katika moja ya barabara zilizopo katikati ya Mji wa Sumbawanga wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jana. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Salum Mohammed Chima na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Sabas Katepa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akijumuika na wa wananchi pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali katika ufagiaji wa barabara za Manispaa ya Sumbawanga.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akifanya uhamasishaji wa usafi wa mazingira katika Mji wa Sumbawanga kwa abiria wa daladala jana kwenye uzinduzi wa kampeni ya "SUMBAWANGA NG'ARA 2012". Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa.

Uhamasishaji huo ulifanyika kwa wananchi wote wakiwemo wapita njia.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitoa mchanga kwenye mtaro katika moja ya barabara zilizopo katikati ya Manispaa hiyo ya Sumbawanga huku Mvua ikiendelea kunyesha.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (kulia) akifagia kwenye moja ya barabara za Mji wa Sumbawanga Mkoani humo jana katika uzinduzi wa kampeni ya kusafisha Mji huo ijulikanayo kama "SUMBAWANGA NG'ARA 2012". Kushoto ni Naibu Meya Manispaa ya Sumbawanga, Aurelia Kanyengele.

Waandishi wa habari nao walikuwepo kutaka kujua kilichomsukuma Mkuu wa Mkoa huo kuamua kuingia barabarani na kuanza kufagia, ambapo alisema Kiongozi bora ni lazma afanye kazi kwa vitendo na kuwa mfano bora kwa wale anaowaongoza.

Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Frank Maten akijumuika kwenye kampeni hiyo.

Wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga walihamasika na kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika kampeni hiyo.

4 comments:

  1. Wapelekeshe hao na wa Dar waige mfano sio kujifungia maofisini wakati jiji limeoza. Nafikiri hii kampeni isambae nchi nzima!

    ReplyDelete
  2. hongera Injinia na mhe. mbunge kwa kuonyesha njia

    ReplyDelete
  3. Habari za kazi mimi huwa ni msomaji ya blog hii na nimeguswa sana na utendaji kazi ya mkuu wa mkoa wa sumbawanga.Huyu Mheshimiwa ni mfano mzuri wa uongozi bora ambao nchi hii inahitaji viongozi wanaongoza kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa.Ushahidi unaonyesha Mkubwa wa serikali akishika ufagio na kufagia barabara na kuingia ndani ya mtaro kuondoa maji machafu, hawa ndio viongozi ambao tunawahitji watuongoze.Mungu akubariki sana mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Sumbawanga.Sisi watanzania wenzako tunatambua jinsi unafanyakazi kwa bidii.WEWE NI MFANO MZURI UNAOFAA KUIGWA.Serikali iangalie viongozi wa aina hii ili kuwapa nafasi nyeti kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.

    ReplyDelete