Saturday, February 18, 2012

AKIWA ZIARANI MKOANI RUKWA MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MTAFITI BIGWA WA SOKWE DUNIANI AMBAYE PIA NI MTAALAMU WA MAZINGIRA JANE GOODALL IKULU NDOGO YA MPANDA

Si mwingine bali ni Dkt. Jane Goodall ambaye ana zaidi ya miaka 73 mwanamama mtafifiti bigwa wa masokwe duniani kutoka Uingereza ambaye pia ni mtaalamu wa mazingira kwa pamoja Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal anayeonyesha kitabu cha mwanamama huyo kiitwacho "Reason for Hope" kwa baadhi ya waandishi wa habari waliojumuika nao kwenye chakula cha jioni Ikulu ndogo ya Mpanda jana. Mama Jane ametumia zaidi ya miaka 40 ya utafiti wake katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyopo Mkoani Kigoma akitafiti maisha na tabia za Sokwe wanaopatikana kwa wingi katika mbuga hiyo.
.
Mtafiti Jane Goodall akimuonyesha Mhe. makamu wa Rais moja ya tabia za nyani ambayo ni salamu inayotumiwa na mnyama huyo ambaye hushika kichwa kama ishara ya maamkizi. Dkt. Jane Goodal pia ni balozi wa mazingira na viumbe hai duniani katika kuhamasisha umuhimu wa uhai wa vitu hivyo pamoja na ustawi misitu.
Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bllal akishika mdoli wa nyani ambao unamilikiwa na Mama Jane Goodgall  kwa takribani miaka 15 sasa. Alisema kuwa anamiliki mdoli huo kutokana na hisia zake juu ya nyani ambao amekuwa akiwatafiti katika kipindi chote cha maisha yake.
Mama Asha Billal Mke wa Makam wa Rais na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakiwa wameshikilia mdoli huo ambao kwa hakika anavutia pamoja na historia yake.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt. Rajab Rutengwe naye hakuwa nyuma kwani alimtia mkononi mdoli huyo wa kihistoria.
Dkt. Jane Goodall akikumbatiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kabla ya kuondoka katika Ikulu hiyo ndogo ya Mpanda jana usiku.
Picha ya pamoja kati Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal na Dkt. Jane Goodal. Kulia kwa Makamu wa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, wa pili anayefuata na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima. Kushoto kwa Dkt. Jane Goodall ni Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt. Rajab Rutengwe.

No comments:

Post a Comment