Wednesday, February 15, 2012

KUTOKA RUVUMA LEO: MAKAMU WA RAIS ATOA TAMKO KUHUSU MRADI WA URANIUM - NAMTUMBO

Makamu Rais DKT Mohamed Ghalib Bilal akihutubia mamia ya wananchi wa kijiji cha Likuyu sekamaganga wilaya ya Namtumbo wakati alipofanya ziara katika mradi wa urani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewahakikishia wakazi wa mkoani Ruvuma na Tanzania kuwa mradi wa mgodi tarajali wa Urani wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma utatekelezwa kwani una umuhimu kwa taifa.
Amesema hayo wakati akiongea na wafanyakazi wa mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Mantra Tanzania kuwa serikali inafuatilia kwa makini kuona madini haya muhimu ya nalifaidisha Taifa
Aliongeza kuwa anao uhakika kuwa taratibu zote za hifadhi ya mazingira na usalama wa maisha ya wakazi wan aozunguka eneo hilo umetiliwa mkazo nwa Kampuni kwa kushirikiana na taasisi ya nishati ya atomiki Tanzania
.Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa Mantra Tanzania Asa Mwaipopo ameiomba serikali kuharakisha taratibu za kisheria ili mgfodi uweze kuanza hapo mwaka ujao kwa ujenzi na ifikiapo 2014 uzalishaji uanze ili ajira zipatazo 1600 wakati wa ujenzi wa mgodi na zingine 400 wakati wa uzalishaji ziweze kupatikana kwa watanzania na kusaidia kukuza uchumi.
Makamu wa Rais ya sampuli za urani kutoka kwa mjiolojia wa kampuni ya Mantra Emauel Nyamusika(kulia) wakati alipotembela mgodi tarajali.
 
Makamu wa Rais akipokewa na viongozi wa kampuni ya Mantra wakati alipowasili katika eneo litakalojengwa mgodi wa Uranium wilaya ya Namtumbo.  (Picha na Revocatus A.Kassimba ofisi ya mkuu wa mkoa Ruvuma)

No comments:

Post a Comment