Monday, February 13, 2012

MABALOZI WANAOWAKILISHA TANZANIA NJE YA NCHI WATEMBELEA NYUMBANI KWA WAZIRI MKUU KIJIJI KWAO WILAYANI MPANDA JANA

 Baadhi ya Mabalozi wanaowaiwakilisha Tanzania nje ya nchi wakiwa katika picha ya pamoja na mama mzazi wa Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, Albetina Kasanga (wa pili kushoto) na mdogo wake Waziri Mkuu Wolfgang Pinda (kulia) Kijijini kwao Kibaoni wilayani Mpanda jana. Waliosimama kutoka kushoto ni balozi Dkt.James Alex Msekela (Italia) Balozi Dkt.Diodorus Kamala (Ubeligiji) Dkt. Ladislaus Komba (Uganda) na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt.Rajab Rutengwe, Waliokaa kushoto ni Balozi Philipo Marmo (China) na Balozi Mohamed Hamza (Misri). Mabalozi hao wako katika ziara ya kutembelea Hifadhi za Taifa ya Katavi iliyoandaliwa na TANAPA kuongeza uelewa wa kuvutia watalii katika nchi wanazowakilisha.

Balozi wa Tanzania nchini Ubeligiji, Dkt.Diodorus Kamala akiagana na Mama mzazi wa Waziri Mkuu, Albetina Kasanga mara baada ya kutembelea familia hiyo katika kijiji cha Kibaoni wilayani Mpanda Mkoa mpya wa Katavi jana, kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dk James Alex Msekela na nyuma ni Balozi wa Tanzania nchini Misri Mohamed Hamza. Picha na Filbert Rweyemamu.

No comments:

Post a Comment