Saturday, February 18, 2012

MAKAMU WA RAIS AWASILI WILAYANI MPANDA LEO KWA ZIARA YA SIKU 7 MKOANI RUKWA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Billal akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda leo kwa ziara ya kikazi ya siku saba Mkoani Rukwa.

Mhe. Makamu wa Rais akisalimiana na wananchi wa Mpanda mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mpanda tarayi kwa kuanza ziara yake ya siku saba Mkoani Rukwa. Anayeongozana naye kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya. Makamu wa Rais anategemea kufanya ziara yake katika wilaya zote tatu za Mkoa wa Rukwa ikiwepo Mpanda yenyewe, Nkasi na Mpanda ambapo atahitimisha ziara hiyo tarehe 24 Februari na kuelekea Mkoa jirani wa Mbeya

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye uwanja wa kashaulili wilayani Mpanda. Miongoni mwa mambo aliyosisitizia katika mkutano huo ni pamoja ujenzi wa mabweni katika shule za Sekondari kwa ajili ya wasichana kusaidia kuwaepusha na mimba za mashuleni. Aidha alisisitiza kuhusu upandaji miti kuepukana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

No comments:

Post a Comment