Friday, February 24, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILLAL AZINDUA KAMPENI YA USAFI KATIKA MJI WA SUMBAWANGA LEO NA KUKABIDHI VIFAA VYA USAFI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Billal akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Kampeni ya usafi katika Manispaa ya Sumbawanga ijulikanayo kama "Sumbawanga Ng'ara". Kampeni hiyo ilianzishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Rukwa kwa nia ya kuufanya Mji huo uwe wa mfano na wakupendeza. Kushoto kwake aliyeshikilia utepe ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. Kampeni hiyo inaenda sambasamba na Kauli Mbiu ya "Dumisha Usafi wa Mazingira, Dumisha Upandaji Miti na Dumisha Miundombinu Daima".  
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akiweka jiwe la Msingi katika moja ya barabara kuu za Mji wa Sumbawanga sehemu aliyozindulia Kampeni ya usafi kwa Mji wa Sumbawanga. Kushoto ni Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikabidhi vifaa vya usafi kwa kikundi cha usafi cha Manispaa ya Sumbawanga kama sehemu ya Kampeni ya usafi wa Mazingira katika Mji wa Sumbawanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Billal akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kushoto na Mama Asha Billal  mara baada ya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la msingi katika kampeni hiyo. Pembeni kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal.

Mama Asha Billal Mke wa Makamu wa Rais akifagia katika moja ya barabara za lami katika Mji wa Sumbawanga kama ishara ya kuhamasisha wanawake kushiriki kwenye usafi wa Mji huo.
Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal akiwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa kampeni hiyo. Mhe. Aeshi alieleza kero kubwa ya wananchi wa jimboni kwake kuwa ni Maji na kumuomba Mhe. Makamu wa Rais kuifanyia kazi kero hiyo. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kalambo Josephat Kandege.

Baadhi ya wananchi waliokusanyika katika uzinduzi wa kampeni hiyo.
Makamu wa Rais akiagana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Salum Mohammed Chima mara baada ya majumuisho ya ziara yake katika ukumbi wa manispaa ya Sumbawanga. Makamu wa Rais ameondoka leo Mkoani Rukwa na kuelekea Mkoa jirani wa Mbeya ambapo atakuwa na ziara ya kikazi.

No comments:

Post a Comment