Friday, February 3, 2012

SIKU YA SHERIA NCHINI MKOANI RUKWA YAFANA, KESI MBILI ZA MAUAJI ZA WASHTAKIWA KINAMAMA ZASIKILIZWA NA KUTOLEWA HUKUMU LEO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akitoa neno lake la shukrani katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kushoto ni Mhe. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga G.K. Rwakibarila na Mhe. Jaji Pellagia Khaday wa Mahakama hiyo.  
 Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Kanali John Mzurikwao, Mhe. Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga G. K. Rwakibarilla, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya, Mhe. Jaji Pellagia Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, na Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Sumbawanga Prosper Rwegerera wakiangalia Kwanya iliyokuwa ikitumbuiza katika Sherehe za Siku ya Sheria Nchini Leo.
 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. G.K. Rwakibarila akikaribishwa kukagua Gwaride maalum lililoandaliwa kwa heshma yake katika kuadhimisha Siku ya Sheria Nchini Mkoani Rukwa Leo.

Mhe. Jaji Mfawaidhi G. K. Rwakibarila akikagua Gwaride hilo.
Gwaride maalum lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa kufanikisha Siku ya Sheria Mkoani humo likitoa salam za heshma kwa Jaji Mfawaidhi Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga mara baada ya kukaguliwa.

 Mhe. Jaji Mfawidhi akiteta jambo na wenzake mara baada ya kukagua Gwaride la heshma.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Jaji Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga wakijumuika kwenye kwaya. 

 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akijumuika kupanda Mti katika eneo la Mahakama hiyo katika kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Sheria.

 Jaji Mfawidhi Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. G.K. Rwakibarila akipanda Mti katika eneo la Mahakama hiyo katika kufanikisha Siku ya Sheria Nchini na Uhifadhi wa mazingira.
 Jaji Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga akijumuika kwenye zoezi la upandaji Miti.
Menaja wa Sido Mkoa wa Rukwa Ndugu Martin Augustino Chang'a akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao kupanda Miti.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, katibu wake Frank Mateny (kushoto), Afisa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Rukwa George Kiria na Mpelelezi Mkuu wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Rukwa wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga wakisubiri kuanza kusikiliza mashauri yaliyopangwa kusikilizwa katika mahakama hiyo yaliyombatana na maadhimisho ya Siku ya Sheria Nchini.
Mawakili wa Serikali na waupande wa utetezi wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga wakimsubiri Jaji Mfawaidhi wa Mahakama hiyo aingie kwa ajili ya kushughulikia mashauri ya watuhumiwa waliohukumiwa kwa kupewa adhabu mbadala kama kauli mbiu ya Siku ya Sheria inavyosema kuwa ni "Adhabu Mbadala katika Kesi za Jinai na Faida zake kwa Jamii"
Washtakiwa wawili wanawake mmoja aliyeshtakiwa kwa mauaji ya kichanga (mwanae) ajulikanaye kwa jina la Rose Membeye, na Bi. Kiiliana aliyeshtakiwa kwa mauaji ya mumewe Edgar bila kukusudia. Wote hao wawili wamehukumiwa leo na Jaji Mfawidhi Mahakama kuu Kanda ya Sumbawanga Mhe. G.K. Rwakibarila adhabu mbadala ya mwaka mmoja nje chini ya uangalizi maalum wa Afsa Ustawi wa Jamii kwa masharti ya kutokutenda kosa lolote kwa kipindi cha mwaka huo mmoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongozana na Jaji Khaday wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga mara baada ya zoezi la upandaji miti katika eneo la mahakama hiyo. Mahakama hiyo imepiga hatua kubwa katika uhifadhi wa mazingira na upandaji miti. Kwa faida ya wasomaji wawili hao walisoma pamoja Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea (O-Level). 

No comments:

Post a Comment