Friday, February 10, 2012

UJENZI WA KITUO CHA AFYA INYONGA WAENDELEA, KUWEKWA JIWE LA MSINGI NA MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILLAL TAREHE 19/02/2012


Kituo cha Afya Inyonga ambacho kipo wilayani Mpanda ni miongoni mwa kituo kikubwa cha afya Mkoani Rukwa kinachojengwa kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Serikali ya Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete alizozitoa wakati wa uchaguzi. Jengo linaloonekana kwa nje ni wodi za kulaza wagongwa katika kituo hicho.

Kituo hiki kitawekwa jiwe la msingi na Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal ambaye atakuwa Mkoani Rukwa kwa ziara ya siku 7 kuanzia tarehe 18-24/ 02/2012. Ziara hiyo itajumuisha mikoa miwili ambayo ni Rukwa yenyewe na Mkoa mpya wa Katavi. Katika ziara yake hiyo amepangiwa kutembelea wilaya zote tatu za Mpanda, Nkasi na Sumbawanga ambapo atapokea taarifa mbalimbali za miradi ya maendeleo, uzinduri wa miradi hiyo pamoja uwekaji wa jiwe la msingi kwenye miradi ambayo inaendelea kujuengwa.

Huduma za vyoo, bafu na sehemu za kupumzikia wagonjwa na wageni zimetengwa katika wodi hizi za wagonjwa.
Hizi ni wodi za wagonjwa kwa ndani ya jengo hilo. Ujenzi ukikamilika vitanda vitawekwa kwenye vichumba vinavyoonekana.
Sehemu ya kunawa mikono. Ujenzi bado unaendelea.

Baadhi ya sehemu ndani ya jengo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya alitembelea kituo hicho tarehe 29/02/2012 kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. Alipiga picha ya pamoja na mafundi wanaojenga kituo hicho. Mkuu huyo wa Mkoa alitoa maagizo kwa mkandarasi anayejenga kituo hicho kubadilisha tiles za kichina ambazo zimetumika kwenye baadhi ya sehem katika jengo hilo kwa madai kuwa baada ya muda mfupi zinapoteza ubora wake.

Consultation Block.

Consultation Rooms.

No comments:

Post a Comment