Sunday, March 4, 2012

INJINIA STELLA MANYANYA AZINDUA RASMI HARAMBEE YA KUCHANGIA MLIMANI TV, ACHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 30, AWAOMBA WADAU KUZIDI KUCHANGIA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Songea kupitia tiketi ya CCM na Mjumbe wa bodi ya baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa kazini kuendesha harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kituo cha Mafunzo na Utangazaji cha Mlimani TV jana. Aliweza kuchangisha zaidi ya Milioni 30. Injinia Manyanya amezindua harambee hiyo jana ambapo amewaomba wadau kuendelea kuchangia kwa maendeleo ya habari nchini. (Picha na Hamza Temba)
Baadhi ya wafanyakazi na wadau wa taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakitoa mchano wao, hapo wakiongozwa na Associate Dean Mr. Irigo. Kulia akiwa muendesha harambee hiyo Injinia Stella Manyanya.
Baadhi ya wanafuni wa Undergraduate katika taasisi hiyo wakitoa mchango wao wakiongozwa na Rais wao anaezungumza kwenye Mic. Kulia akiwa muendesha harambee hiyo Injinia Stella Manyanya
Baadhi ya wadau waliohudhuria harambee hiyo wakifuatilia moja ya matukio katika hafla hiyo

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Yunus Mgaya akimkabidhi zawadi ya ukumbusho (Wheel Cover ya Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma) Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kama shukurani kwa ushirikiano wake katika kuendesha gurudumu la maendeleo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma Profesa Bernadikta Kilian na Meya wa Manispaa ya Kionondoni Yusuf Mwenda. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliaga kwenye hafla hiyo kwa kulifungulia Rumba kama inavyoonekana pichani. Wengine walioungana nae ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Yunus Mgaya, Mkuu wa Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma Profesa Bernadikta Kilian na Meya wa Manispaa ya Kionondoni Yusuf Mwenda.

Na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Songea kupitia tiketi ya CCM na Mjumbe wa bodi ya baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amewaomba wapenda maendeleo ya vyombo vya habari nchini ikiwepo Serikali, Mashirika ya umma, Taasisi binafsi , Makampuni na watu binafsi kuchangia kuboresha kituo cha Televisheni cha Mlimani TV kinachomilikiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo jana kwenye hafla ya kusherehekea mafanikio ya vyombo vya habari vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuukaribisha mwaka mpya 2012 wakati akizindua mpango endelevu kwa ajili kuchangia kituo hicho (Fund Rising) uliyofanyika katika Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (IJMC) na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ya vyombo vya habari nchini.
Zaidi ya shilingi milioni 30 zilipatikana jana ambapo fedha taslimu zilikuwa alfu 50 na ahadi zikiwa zaidi ya milioni 30. Harambee hiyo iliongozwa na Mhe. Manyanya ambaye binafsi alichangia shilingi milioni moja akiwa kama mjumbe wa baraza kuu la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mdau mkubwa wa vyombo vya habari nchini.
Wengine waliochangia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Yunus Mgaya ambaye alichangia shilingi Milioni moja na Mkuu wa Chuo hicho Profesa Bernadikta Kilian ambaye alichangia shilingi laki sita. Wengine baadhi waliochangia ni walimu wa chuo hicho, wanafunzi, Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Ilala, Home Shopping Centre na Ubalozi wa Marekani waliochangia shilingi milioni 15.
Injinia Manyanya alisema kuwa kuna haja kubwa ya kuboresha Studio ya Mlimani TV na vyombo vyake vya kufundishia kutokana na umuhimu wa chuo hicho nchini kwa ajili ya kuzalisha waandishi wa habari bora kwa kuzingatia misingi ya taaluma. Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndiyo taasisi pekee ya Umma inayotoa mafunzo ya Uandishi wa habari nchini.
"Tuungane pamoja kuhakikisha vifaa vinavyohitajika vinapatikana kwani leo hii tunazindua mkakati wa kuchangia kuiwezesha taasisi hii iweze kuendesha shughuli zake kwa kufuata ueledi wa tasnia ya vyombo vya habari nchini kwa kuzalisha pia waandishi bora na sio bora waandishi. Hiyo ni kutokana na umuhimu wa waandishi wa kwani wana uwezo mkubwa wa kutumia taaluma yao kuleta amani au vurugu katika nchi" Alisema Injinia Manyanya.
Hapo kabla Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Yunus Mgaya alisema kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kina Mpango mkakati wa miaka 50 ijayo ambapo lengo lake kubwa ni kuimarisha miundombinu na kuboresha vipindi vya taaluma ambapo alikiri kuwa zoezi hilo hawataweza kulifanya wenyewe jambo lililowalazimu kuzindua mkakati huo wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kufikia malengo hayo.

No comments:

Post a Comment