Thursday, March 15, 2012

KIKAO CHA 23 CHA KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA (RCC) CHAKUTANA JANA NA KUJADILI MAMBO MBALIMBALI NA KUFIKIA MAAZIMIO KWA AJILI YA UTEKELEZAJI


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa maneno ya ufunguzi kwenye kikao cha 23 cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC). Kikao hicho kilifanyika jana kwenye ukumbi wa RDC uliopo katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali, viongozi, wageni waalikwa na waandishi wa habari. 

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndg. Alhaj Salum Mohammed Chima ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa akitoa neno la awali na kumkaribisha Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanaya aweze kufungua kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho, Ignas Malocha Mbunge wa Jimbo la Kwela, Ally Kessy Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, na Suleiman Kakoswe Mpanda Vijijini wakifuatilia kikao hicho.
Makatibu Tawala wa Wilaya ya Sumbawanga (Salum Shilingi), Nkasi (Josephat Kakuru) na Mpanda (Lauten Kanon) wakifuatilia kikao hicho.

Mhariri wa Blogu ya Rukwereview Hamza Temba na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Samson Mashalla na wajumbe wengine wakifuatilia agenda mbalimbali za kikao hicho.

Sekretatieti ya Kikao hicho ikiwa kazini kuhakikisha kumbukumbu zote za kikao hicho kinaingia kwenye karatasi zao. Kutoka kulia ni Florece Chrissant, Festo Chonya na Abubakar Serungwe.

Meneja wa Sido Mkoa wa Rukwa Martin Augustino Chang'a akiwa anafuatilia kwa umakini kikao hicho. Wengine ni baadhi ya wataalamu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa. 


Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dkt. Rajab Rutengwe akiteta jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima katika kikao hicho.  
Baadhi ya wajumbe na wageni waalikwa wa kikao hicho wakisikiliza neno la ufunguzi wa kikao hicho likitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (hayupo pichani). 
Waandishi wa Habari wakichapa kazi huku kikao kikiwa kinaendelea, Peti Siyame Daily News na Habari Leo na Mussa Mwangoka (Mwananchi-kulia), wengine hawapo pichani.

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Mipango David Kilonzo akiwasilisha moja taarifa katika kikao hicho.

No comments:

Post a Comment