Friday, March 16, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AMPONGEZA DKT. RAJAB RUTENGWE KWA KUTEULIWA KUWA MKUU WA MKOA MPYA WA KATAVI LEO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkumbatia Dkt. Rajab Rutengwe kama ishara ya pongezi kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Rutegwe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ambayo ilikuwa ndani ya Mkoa wa Rukwa ambao sasa utakuwa na Wilaya ya Sumbawanga, Nkasi na Wilaya mpya ya Kalambo. Katavi itakuwa na Wilaya ya Mpanda na Wilaya mpya ya Mlele.  Injinia Manyanya hakusita kuelezea furaha yake kwa kusema kuwa "Rukwa imejifungua Katavi na Mimi nimejifungua Dkt. Rajab Rutengwe, Hakika ni furaha kubwa kwetu kwani sote tulikuwa tunamuombea ili tuweze kudumisha ushirikiano tuliokuwa nao wa Wanarukwa na Katavi ,Shukrani kwa Mhe. Rais kwani ndoto yetu imetimia"  Alisema Mhe. Manyanya.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa na Mkuu wa Mkoa mteule wa Mkoa mpya wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe alipomtembelea Ofisini kwake leo asubuhi.  Dkt. Rutengwe ni miongoni mwa wakuu wa Mikoa wapya wanne walioteuliwa jana na Mhe. Rais Dkt. Jakaya Kikwete. Wengine ni Ndugu Magalula Saidi MAGALULA Mkoa wa GEITA kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Ndugu Paschal Kulwa MABITI Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida na Kapt. Asery MSANGI Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE kabla ya hapo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.

No comments:

Post a Comment