Saturday, March 17, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AMUAGIZA MKURUGENZI WA MANISPAA YA SUMBAWANGA NA MKANDARASI "KMM" ANAYEJENGA BARABARA ZA LAMI KATIKA MANISPAA HIYO KUJENGA MIUNDOMBINU HIYO KWA UBORA ZAIDI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa kwenye kikao na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga William Shimwela na Timu yake ya Manispaa pamoja na Timu ya wakandarasi wa Kampuni ya KMM inayojenga barabara za lami katika Manispaa ya Sumbawanga. Mkuu huyo wa Mkoa aliamua kuonana na timu hiyo kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya miundombinu ya barabara kujengwa kwa kiwango cha chini. Hata hivyo Mkandarasi huyo aliahidi kufanya marakebisho kwa maeneo ambayo yanawezekana kufanya hivyo. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa aliahidi kusimamia zoezi hilo kikamilifu kuhakikisha Manispaa inakuwa na miundombinu bora. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stela Manyanya akimuonyesha mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Ndugu William shimwela na wakandarasi wanaojenga barabara za lami katika Mji wa Sumbawanga kipande cha lami katika barabara iingiayo katika Ofisi ya Mkuu huyo kinachoendelea kumegwa na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Rukwa na kuwaagiza kuhakikisha wanajenga miundombinu bora ili iweze kuwa na manufaa ya kudumu. Baadhi ya barabara katika Mji wa Sumbawanga zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi kwa sababu mbalimbali jambo lililomlazimu Mkuu huyo wa Mkoa kukutana na Viongozi wa Manispaa na Wakandarasi kujadili hatma ya barabara hizo

No comments:

Post a Comment