Friday, March 9, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA MAJIMAJI LEO


Kikundi cha ngoma cha Better Life cha Songea kikimkaribisha kwa nyimbo za asili za kabila la wangoni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Songea kwa tiketi ya CCM alipotembelea Makumbusho ya Taifa ya Majimaji leo. Katika ziara yake hiyo alipata kuona kaburi walilozikwa mashuja 66 walionyongwa na wajerumani  mwaka 1906 wakati wa vita ya Majimaji. Alipata kuona pia Onyesho maalum la marehemu Dkt. Laurence Mutazama Gama aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Ruvuma kwa vipindi tofauti. Dkt. Gama alikuwa Mngoni wa kutoka familia ya kichifu ya kabila hilo.
Mkuu wa Kikundi cha ngoma cha Better Life Mama Munagama akikabidhi zawadi ya mbuzi na mchele kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kama shukrani kwa kiongozi huyo kukipeleka kikundi hicho Dar es Salaam kwenye Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania lililowasilishwa na Jamii za Wanarukwa na Katavi  mwishoni mwa mwaka jana. Kushoto ni Afisa Habari na Mahusiano Mkoa wa Rukwa Hamza Temba na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Balthazar Nyamusya.
Ni heshma kubwa kwa Utamaduni wa kabila la wangoni wacheze ngoma zao kwa kulala chini, heshima hiyo alipewa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na kikundi cha Ngoma cha Better Life kama inavyoonekana pichani wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipotembelea makumbusho ya taifa ya Majimaji leo.


Wakwanza ni Mama Siwajali Gama mke wa marehemu Dkt. Laurence Gama aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Ruvuma kwa vipindi tofauti. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum (CCM) Songea na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Balthazar Nyamusya wakiwasalia mashujaa 61 wa vita ya Majimaji walionyongwa na wajerumani katika kaburi lao la pamoja ambalo lipo ndani ya Makumbusho ya taifa ya Majimaji. 
Kaburi alilozikwa Nduna wa Songea, Songea Mbano ambalo lipo ndani ya makumbusho ya Taifa ya Majimaji mjini Songea.
Orodha ya mashujaa walionyongwa na wajerumani tarehe 27 Februari 1906 wakati wa vita ya Majimaji Songea Mkoani Ruvuma. Mashujaa wote hao walizikwa katika kaburi moja ambalo lipo ndani ya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji.
Mama Siwajali Gama mke akitoa maelezo ya Onyesho maaluum la historia ya mumewe marehemu Dkt. Laurence Gama aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Ruvuma kwa vipindi tofauti lililowekwa hivi karibuni katika chumba maalum kwenye makumbusho ya hayo. Pichani akitolea maelezo picha na mavazi aliyotumia mumewe wakati wa uongozi wake katika idara tofauti Serikalini. Wanaoshuhudia onyesho hilo ni Injinia Stella Manyanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum (CCM) Songea. Katika Onyesho hilo vipo vitu vingi alivyotumia kiongozi huyo zikiwepo pia medali alizopewa, mavazi, na nishani mbalimbali katika mchango wake Serikalini na Kimataifa.
Miongoni mwa vifaa vinavyoelezea historia ya marehemu Dkt. Gama. Inayoonekana ni ngao pamoja na vyeti alivyopewa marehemu Dkt. Gama Mkoani Tabora kama ishara ya heshma na mchango wake katika uongozi wa Chama Chamapinduzi katika Mkoa huo na taifa kwa ujumla. 
Injinia Manyanya akitoa ushauri kwa Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo ya Taifa ya Majimaji Balthazar Nyamusya kuhusu namna ya kuboresha makumbusho hiyo iweze kuleta tija zaidi. kushoto ni Mama Siwaji Gama mke wa marehemu Dkt. Laurence Gama aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Ruvuma kwa vipindi tofauti

No comments:

Post a Comment