Wednesday, March 14, 2012

RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA CHAMA CHA MADAKTARI WA KINYWA NA MENO LEO, "NATAKA KULIACHA TAIFA LIKIWA NA WATU WENYE AFYA NJEMA" ANENA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa kujadili jinsi ya kuyaweka masuala ya kinywa na meno katika hatua ya awali ya kupata huduma. Jumla wa wajumbe kutoka nchi 18 wanahudhuria mkutano huo wa siku tatu unaofanyika hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais wa chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Nchini Dk. Rachel Mhavile (kulia) na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donnan Mmbando baada ya kufungua mkutano wa siku tatu wa kujadili jinsi ya kuyaweka masuala ya kinywa na meno katika hatua ya awali ya kupata huduma ambapo jumla ya wajumbe kutoka nchi 18 wanahudhuria mkutano huo.
 
RAIS Jakaya Kikwete amesema kwamba serikali itafanya kila iwezavyo katika kupanuana kuendesha huduma za afya zilizobora na kisasa ili kuhakikisha taifa linakuwa la watu wenye afya njema kwa kuzuia na kutibu magonjwa mbalimbali katika kipindi cha uongozi wake.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Rais Kikwete mara baada ya kukabidhiwa kadi ,katiba na tuzo yakukubali kuwa mwanachama wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania na Rais wa chama hicho, Rachel Mhaville katika hoteli ya Court yard jijini DaresSalaam.
“Sikutegemea kutokea kwa kitendo hiki.Ninachoweza kusema ninaomba mniamini nitakuwa mwanachama mzuri. Tutafanyakazi kwa pamoja ili kutimiza ndoto zenu hususan kuhakikisha mradi wa kituo cha Kigamboni cha magonjwa hayo unaanzishwa.
“Hili ni jukumu kwangu , kwani lengo langu ni kuliacha taifa likiwa lenye watu wenye afya njema,” alisema Rais Kikwete.
 
Aliongeza kuwa serikali yakeinafanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha ujenzi wa Chuo Kikuu kipya chaSayansi za Afyana Tiba eneo la Mlongazila unafanikiwa ili kiweze kufanya kazi kabla ya mwaka 2015.
Rais Kikwete alisema chuo hicho kitakuwa na shule mbalimbali za afya na tiba.
Akifungua mkutano wa mafunzo ya siku tatu ya kuweka hatua za awali za kupata huduma za kuzuia na kutibu magonjwa hayo,Rais Kikwete alisema bado kuna safari ndefu ya kuiwezesha sekta ya huduma hiyo kuwa na rasimali watu wa kutosha wakiwemo madaktari, wauuguzi na watumishi wengine wa eneo hilo.
Rais Kikwete aliongeza kuwa sekta hiyo ina upungufu wa madakatari ukilinganisha na idadi ya watu nchini wapatao milioni 43 .
Alizitaja takwimu za madaktari wa sekta hiyo nchini kuwa wapo 518 ambapo uwiano unaonesha kuwa 1: 120,000 (yaani daktari mmoja kwa wagonjwa 120,000) wakati kwa sheria za Shirika la Afya la Dunia(WHO) 1:7500(yaani daktari mmoja anatakiwa kutibu wagonjwa 7500).
“Serikali itaendelea kujenga uwezo kwenye hospitali na kituo cha afya, lazima ziwe na vitengo vya huduma za kinywa na meno,” alisisitiza huku akiongeza kwamba itasaidia kuanzisha na kupanunua vilivyopo na itangaliaili iweze kuanzisha hata katika Chuo Kikuu cha Dodoma.
Alitoa changamoto kwa wadau wa sekta hiyo kuhakikisha kuwa hudumaza magonjwa hayo zinapatiakana, kutolewa katika hatua za awali na kwa gharama nafuu.
Naye Rais wa chama hicho, Mhaville alisema aliitaka jamii kuacha kutembea na magonjwa hayo badala yake wafike hospitali ili kupata ushauri natiba kwa kuwa magonjwa hayo yanazuilika.
Alisema changamoto iliyopo kwao ni kutoa elimu kwa jamii hususan kwenye maeneo ya vijijini.
Mhaville alisema mkutano huo utatengeneza mwongozo wa mamna ya kuyashughulikia magonjwa ya afya ya kinywa na meno, ambapo Rais alisema serikali inausubiri kwa hamu.

NA
MAGRETH KINABO – MAELEZO

No comments:

Post a Comment