Thursday, March 8, 2012

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOANI RUVUMA LEO, INJINIA STELLA MANYANYA ASIKITISHWA NA MGOMO WA MADAKTARI NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Songea kupitia CCM Injinia Stella Manyanya akihutubia wananchi wa Songea leo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambapo hakusita kuonyesha masikitiko yake kwa mgomo wa madaktari nchini ambao alisema unawaathiri zaidi kinamama na watoto. Alisema kuwa leo hii kina mama wangegoma hata hao madaktari wasingekuwepo. Amewaomba madaktari nchini kuacha kutumia njia hiyo ya mgomo kama suluhu ya kutatua madai yao kwani wanaoumia zaidi ni wananchi wasiokuwa na hatia.

Alisema njia salama ni kukaa meza moja na Serikali na majibu yatapatikana kwa kupeana muda na sio kuweka shinikizo. Aliendelea kusema kuwa kitendo cha kumpa Mhe. Rais muda wa kuwaondoa madarakani viongozi aliowateua yeye mwenyewe si kitendo cha heshma kwa kiongozi huyo mkubwa katika nchi. Kwa upande mwingine amesema kuwa angependa kuona madai ya msingi ya madaktari yanafanyiwa kazi kwa ustawi wa sekta ya afya nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya 

Kinamama Oyyeeeee! Wanawake Saafiiiiiii! Muongozaji wa Blogu ya rukwareview Hamza Temba ambaye ni Afisa Habari na Mahusiano Mkoa wa Rukwa alipata fursa ya kusalimiana na Wanawake wa Songea.

No comments:

Post a Comment