Friday, March 9, 2012

WAKUU WA MIKOA YA RUKWA NA RUVUMA WAONANA NA MFADHILI MILLENIUM CHALLENGE COOPEARTION (MCC) KUJADILI MIRADI YA BARABARA INAYOFADHILIWA NA SHIRIKA HILO MIKOANI HUMO JANA MJINI SONGEA

Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa shirika la Millenium Challenge Account  Tanzania Dar es Salaam(MCA-T Dsm) Bw. Bernard Mchomvu akimkabidhi zawadi ya Khanga yenye nembo ya shirika hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya walipoonana ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu (kulia) jana kujadili miradi ya barabara inayodhaminiwa na shirika la Millenium Challenge Cooperation (MCC) kupitia Tanzania Millenium Challenge Account (MCA-T Dsm).

Shirika hilo linafadhili ujenzi wa barabara kuu za lami zinazojengwa Mkoani Rukwa zenye jumla ya Km. 224 kwa miradi ya Tunduma-Ikana, Ikana-Laela, na Laela-Sumbawanga. Kwa mujibu wa Bwana Mchomvu miradi hiyo yote pamoja na changamoto zote kuzingatiwa itakuwa imekamilika ifikapo mwezi June 2013 na barabara zote zitakuwa zimekabidhiwa kabla ya mwezi wa nane 2013.

Kwa upande wa Ruvuma shirika hilo linafadhili ujenzi wa barabara itokayo mjini Songea kuelekea Wilaya ya Mbinga ambapo ujenzi huo unaendelea na unategemewa kukamilika mwakani.

Hata hivo Mkurugenzi huyo aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano wanaoutoa kuwaeleimisha wananchi wao juu ya umuhimu wa miradi hiyo na ulinzi wa vifaa vya ujenzi kwani umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza wizi wa vifaa vya ujenzi vilivyokuwa vinafanywa na baadhi ya wananchi na wafanyakazi wasiokuwa waaminifu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya allishukuru shirika hilo kwa jitihada zao za kuchangia maendeleo nchini. Aliwashukuru pia kwa hatua za hivi karibuni walizochukua kujenga daraja la Laela ambalo ni kiunganishi muhimu kwa wananchi wa eneo hilo katika shughuli zao za kila siku hususani kuwaunganisha na kituo cha afya cha Laela.

Picha ya pamoja kati Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu, Injinia Stella Manyanya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Tarimo na wawakilishi wa Jumuiya ya Millenium Challenge Cooperation (MCC) Bw. Carl Fickenscher Mkurugenzi Mkazi nchini (kushoto) na Bw. Bernard Mchomvu Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa shirika la Millenium Challenge Account Tanzania Dar es Salaam(MCA-T Dsm).
Kushoto Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa shirika la Millenium Challenge Account Tanzania Dar es Salaam(MCA-T Dsm) Bw. Bernard Mchomvu akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.

No comments:

Post a Comment