Tuesday, March 13, 2012

WAWAKILISHI KUTOKA WIZARA YA KILIMO NA CHAKULA WAPO MKOANI RUKWA KUFANYA TATHMINI YA WANUFAIKA WA VOCHA ZA RUZUKU YA PEMBEJEO ZA KILIMO


Wawakilishi kutoka Wizara ya Kilimo na Chakula, kutoka kushoto ni Michael Mahecha Mwenyekiti wa Mawakala nchini, Stella Mlutangwa Mkufunzi Mkuu wa Kilimo na Michael Mayabu, wote hao wapo Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufanya tathmini ya vocha za ruzuku ya pembejo za kilimo ambapo watatembelea baadhi ya vijiji. Wataonana pia na wakulima pamoja na wadau mbalimbali kujua kama walipata vocha na kufanya tathmini ya matokeo ya pembejeo hizo.  

Kwa upande mwingine wawakilishi hao waliupongeza uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa hatua kubwa waliyopiga ya kuhimiza wananchi wake katika kilimo cha wanyamakazi. Mkoa wa Rukwa ni Mkoa pekee unaotumia wanyamakazi kwa zaidi ya 70% katika kilimo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Stella Manyanya akiongea na wawakilishi hao walipomtembelea ofisini kwake jana kutambulisha ujio wao. Mkuu wa huyo wa Mkoa aliwaeleza wawakilishi hao kuwa mpaka sasa zoezi la usambazaji wa vocha za pembejeo za ruzuku ya za kilimo mwaka huu haujakuwa na malalamiko mengi kiasi cha kusema kuwa zoezi hilo limefanikiwa. Changamoto kubwa aliyoitoa kwa wawakilishi hao ni kuendelea kutafuta masoko zaidi kwa ajili ya ziada kubwa ya mazao yanayozalishwa mkoani Rukwa ambayo mwaka jana ilikuwa ni zaidi ya tani laki 4 ya mahindi. 

No comments:

Post a Comment