Wednesday, April 25, 2012

BAADHI COMMENTS ZILIZOTOLEWA NA WADAU WA RUKWAREVIEW NDANI NA NJE YA NCHI TANGU MTANDAO HUU UANZISHWE

1-17 of 17
Anonymous
on 4/18/12
Nampongeza sana sana Mkuu Wa Mkoa Inj.Manyanya kwa uamuzi aliotoa kuhusu uwanja wa ndege wa Kisumba kujengwa badala ya kuendeleza Uwanja uliopo katikati ya mji. napendekeza uwanja wa sasa upimwe viwanja na kupewa Shirika La Nyumba ili zijengwe nyumba za kukopesha na kuuza kwa wananchi kwani shirika la nyumba litajenga nyumba bora nzuri na kuleta sura nzuri ya mji....Tamim Said on FAHAMU ENEO LILILOTENGWA TANGU MWAKA 1984 KWA AJILI YA KUJENGWA UWANJA WA NDEGE KATIKA MJI WA SUMBAWANGA, KUNA HAJA YA ENEO HILI SASA KUENDELEZWA?
Anonymous
on 2/14/12
This RC is doing terrific job. She is great lady and I am impressed with her dedication and hard-work. She makes me remember General T. Kiwelu. on FAHAMU ENEO LILILOTENGWA TANGU MWAKA 1984 KWA AJILI YA KUJENGWA UWANJA WA NDEGE KATIKA MJI WA SUMBAWANGA, KUNA HAJA YA ENEO HILI SASA KUENDELEZWA?
Anonymous
on 1/22/12
Ukijengwa uwanja mpya wa ndege, huo wa sasa utengenezwe kama bustani na eneo la mapumziko. We need open spaces to relax! Nawakilisha. on FAHAMU ENEO LILILOTENGWA TANGU MWAKA 1984 KWA AJILI YA KUJENGWA UWANJA WA NDEGE KATIKA MJI WA SUMBAWANGA, KUNA HAJA YA ENEO HILI SASA KUENDELEZWA?
Anonymous
on 1/22/12
It makes sense to have a new airport in Kisumba. The existing airport is small and it is dangerous for the pedestrians who cross the airport. Mdau wa Edeni A on FAHAMU ENEO LILILOTENGWA TANGU MWAKA 1984 KWA AJILI YA KUJENGWA UWANJA WA NDEGE KATIKA MJI WA SUMBAWANGA, KUNA HAJA YA ENEO HILI SASA KUENDELEZWA?
Anonymous
on 1/22/12
Habari za kazi mimi huwa ni msomaji ya blog hii na nimeguswa sana na utendaji kazi ya mkuu wa mkoa wa sumbawanga.Huyu Mheshimiwa ni mfano mzuri wa uongozi bora ambao nchi hii inahitaji viongozi wanaongoza kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa.Ushahidi unaonyesha Mkubwa wa serikali akishika ufagio na kufagia barabara na kuingia ndani ya mtaro kuondoa maji machafu, hawa ndio viongozi ambao tunawahitji watuongoze.Mungu akubariki sana mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Sumbawanga.Sisi watanzania wenzako tunatambua jinsi unafanyakazi kwa bidii.WEWE NI MFANO MZURI UNAOFAA KUIGWA.Serikali iangalie viongozi wa aina hii ili kuwapa nafasi nyeti kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla. on MKUU WA MKOA WA RUKWA AZINDUA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA MJINI SUMBAWANGA LICHA YA MVUA KUBWA KUNYESHA JANA
Anonymous
on 1/18/12
Habari za kazi mimi huwa ni msomaji ya blog hii na nimeguswa sana na utendaji kazi ya mkuu wa mkoa wa sumbawanga.Huyu Mheshimiwa ni mfano mzuri wa uongozi bora ambao nchi hii inahitaji viongozi wanaongoza kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa.Ushahidi unaonyesha Mkubwa wa serikali akishika ufagio na kufagia barabara na kuingia ndani ya mtaro kuondoa maji machafu, hawa ndio viongozi ambao tunawahitji watuongoze.Mungu akubariki sana mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Sumbawanga.Sisi watanzania wenzako tunatambua jinsi unafanyakazi kwa bidii.WEWE NI MFANO MZURI UNAOFAA KUIGWA.Serikali iangalie viongozi wa aina hii ili kuwapa nafasi nyeti kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla. on MKUU WA MKOA WA RUKWA ATOA ZAWADI YA MWAKA MPYA KWA WAFUGWA WA MAHABUSU MKOANI HUMO
Anonymous
on 1/18/12
Anonymous
on 1/13/12
Wapelekeshe hao na wa Dar waige mfano sio kujifungia maofisini wakati jiji limeoza. Nafikiri hii kampeni isambae nchi nzima! on MKUU WA MKOA WA RUKWA AZINDUA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA MJINI SUMBAWANGA LICHA YA MVUA KUBWA KUNYESHA JANA
Anonymous
on 1/13/12
Anonymous
on 1/13/12
Shukrani kwa taarifa hizi na zingine unazoweka katika blogu hii. Navutiwa kuona taarifa za mkoa ambao sijawahi kufika na taarifa zake hazikuwa zinapatikana kirahisi, hata mtandaoni. Sasa mambo ni mazuri kutosha. Napenda tu nigusie hili suala la hao waTuruki kuagiza vyakula kutoka nchini kwao. Ni kweli, ingekuwa bora wanunue vyakula hapa hapa Tanzania. Mimi ni mtafiti na mwandishi katika masuala ya tofauti za tamaduni hapa duniani. Suala la chakula linapambanua utamaduni moja na mwingine. Hata kwetu ni hivyo hivyo. Vyakula vya Mchagga, kwa mfano, kwa ujumla ni tofauti na vile vya Mpemba. Sasa hao wa-Turuki isije ikawa wanaagiza kutoka kwao kwa msingi huo. Ingefaa tupate taarifa zaidi. Mwarabu akiwa hapa Mpanda, sitashangaa akiagiza tende kutoka Arabuni. Pamoja na kuwa ingekuwa vema iwapo hao wa-Turuki wangenunua vyakula vya kwetu, kuna pia jambo ambalo tunaweza kujifunza kutoka kwao. Mimi ni m-Tanzania ambaye niko hapa ughaibuni, lakini huwa natafuta vyakula kwenye maduka ya on YALIYOJIRI KATIKA ZIARA YA MKUU WA MKOA WA RUKWA WILAYANI MPANDA HIVI KARIBUNI
on 12/26/11
Anonymous
on 11/29/11
Naishukuru sana serikali kwa jitihada zake za uwekezaji nchini Tanzania. Hii inaonyesha nia njema kabisa na thabiti ya kuwainua wananchi wake kwa kipato.Pamoja na shukrani hizi naona kuna sababu za msingi za kuangalia aina ya uwekezaji tunaouruhusu kwenye maeneo husika na athari zake kwa wananchi wetu. Nasema hivi kwa sababu uwekezaji ambao serikali imeuridhia wa Mpanda ambao ni kwenye sekta ya kilimo naona unaathari kwetu. Dunia kwa sasa imekuwa na tatizo kubwa sana la kiuchumi. Mtikisiko ambao sasa unazikumba nchi za Ugiriki, Italia, Marekani, Ufaraansa, Uingereza na nchi nyingine zinazotumia sarafu ya euro ungetumik kama sababu ya kutufanya tukajifunza na sisi pamoja na umasikini wetu. Uzalishaji wa mazao ya chakula kwenye nchi za ulaya ni mdogo na una gharama kubwa sana za uzalishaji. Wakulima wanatumia mtaji mkubwa zaidi kuliko wanachopata na hivyo kufanya mazao yao kuuzwa kwa bei ya ghali sana. Sasa wanakuja kwetu kuwatumia raia wetu kuzalisha kwa gharama ndogo na hivyo kupata on HAKUNA MAENDELEO BILA UWEKEZAJI - RAIS KIKWETE
on 11/12/11
Tunakupongeza sana mheshimiwa Njoolay kwa kazi yako nzuri iliyotukuka ya kuuongoza mkoa wa rukwa. Upendo,uchapakazi na moyo wako wa ukarimu ulioonyesha wanarukwa tutazidi kukukumbuka daima. Umekuwa nasi katika shida na raha na daima ulikuwa mstari wa mbele jutusaidia na kutuongoza. Unaondoka rukwa lakini tunakukaribisha sana rukwa. Eng Manyanya karibu rukwa mkoa wenye fursa nyingi za maendeleo. Ahsante George - UK on ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA RUKWA AAGWA RASMI
on 11/12/11
Naanza sasa kuingiwa na matumaini makubwa sana kwenye mwelekeo mzima wa wanarukwa kwenye ulimwengu wa utandawazi. Fursa hii imechelewa kutufikia kwa kweli. Tumekuwa na historia nyingi japo zimekuwa zikivalishwa gamba la kutisha mfano Uchawi,mazingaombwe,uganga wa jadi nk. Sasa naingiwa na furaha kwani maana halisi ya tafsiri hizo haikuwa kama unavyotakiwa kuwa. Huo ni utamaduni wetu na ndio asili yetu wana rukwa.Makabila mengine yamekuwa yakijitokeza tangu zamani sana na sasa wamekuwa mbali sana na sanaa zao zimekuwa kwenye makumbusho na kununuliwa kwa thamani kubwa sana. Nakuombea mafanikio mema mkuu wa mkoa na wana rukwa kwa ujumla Ahsante sana. George Nkwera - UK on MKUU WA MKOA WA RUKWA ACHANGISHA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 3.9 KUFANIKISHA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MWANARUKWA LITAKALOFANYIKA TAREHE 25-27 NOVEMBA 2011
on 11/12/11
Nakushukuru sana kwa kutuhabarisha habari hizi muhimu sana kwa maendeleo yetu wana rukwa. Binafsi naona kumekuwa na jitihada nzuri sana upande wa serikali na taasisi zake katika kusukuma maendeleo ya rukwa tatizo naliona ni upande wa mwananchi mmojammoja. Watu bado tunaendeleo kugubikwa na blanketi la kihistoria kuwa rukwa ni mkoa usio na maendeleo. Mengi yamefanyika na mazuri sana. jitihada zielekezwe kwenye uhamasishaji wa watu kuongeza bidii katika kufanya kazi za maendeleo na kujitolea. Uamuzi wa kupeleka sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru kimkoa wilayani Nkasi naupongeza sana kwani hii itakuwa fursa kwa wana nkasi kujivunia na kujikumbusha tulikotoka wapi tupo na wapi tunataka Nkasi,Rukwa na Tanzania kwa ujumla tunataka tuwe miaka 50 ijayo. Mkuu wa Wilaya mama Mgana jitihada zake wote tunazijua katika kuhimiza maendeleo ya wilaya na mkoa kwa ujumla. Ahsante sana na endelea kutuhabarisha hususan sisi ambao tuko nje ya nchi kwa sasa. George Nkwera Sumbawanga - on KILELE CHA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU MKOA WA RUKWA KUFANYIKA WILAYANI NKASI
on 11/12/11
Nawashukuru sana wajasiriamali wa Rukwa na wengine ambao wamejitokeza kwenye maonyesho ya SIDO Sumbawanga kuonyesha ubunifu wao na jitihada zao za kujikwamua kiuchumi.Hii ni nafasi ya kuonekana na kujitambulisha kwenye mtandao wa masoko ndani ya nchi na kwingineko duniani. Nawatakia mafanikio mema katika maonesho George Nkwera Sumbawanga - kwa sasa UK on NAIBU WAZIRI VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA SIDO YA NYANDA ZA JUU KUSINI MKOANI RUKWA
 
on 11/12/11
 
HATA WEWE UNAWEZA KUTOA MAONI YAKO YENYE NIA NJEMA NA MKOA WETU PAMOJA NA MTANDAO WETU HUU KWA LENGO LA KUJENGA NA KUBORESHA. TUMIA LUGHA SAFI ISIYOCHAFUA HALI YA HEWA.
 
NAMNA YA KUTOA MAONI/ COMMENTS:
 
Chini ya kila POST utaona sehemu imeandikwa Comments, Bofya hapo mara moja, Shuka hadi chini ya hiyo POST utaona kisanduku kimeandikwa Post a Comment kama kinavyoonekana hapo chini.

0 comments:

Post a Comment


 
 
Andika Comments/ maoni yako hapo unaweza kuandika jina na contact zako kama ukipenda kisha chini ya hicho kisanduku utaona maneno haya "  " Uchaguzi upo kwenye hicho kimshale kinachoangalia chini, chagua "Annonymus" kisha nakili maneno utakayopewa yaliyoandikwa kwa kificho kwenye kisanduku kinaochoonekana alafu Bofya Publish. Comment yako itakuwa hewani popote duniani katika mtandao huu na itaifikia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa, kama inahitaji kufanyiwa kazi basi itafikishwa kwa wahusika na kufanyiwa kazi. Nawatakia kazi njema na Afya Bora.

No comments:

Post a Comment