Thursday, April 19, 2012

FAHAMU FUKWE ZA UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA MKOANI RUKWA ZILIZOHIFADHIWA KUVUTIA WAWEKEZAJI KATIKA UKANDA WA ZIWA TANGANYIKA

Ukanda wa Ziwa Tanganyika unajumuisha mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma. Mikoa hii kwa pamoja ni Mikoa iliyopitiwa na Ziwa Tanganyika ambalo fukwe zake ni sehemu ya Utawala katika Mikoa hiyo. Ziwa hilo kwa upande wa pili limepakana na Nchi jirani za Kongo, Zambia na Burundi pamoja na Rwanda. Miongoni mwa fursa kuu zinazopatikana humo ni pamoja na uvuvi, usafirishaji katika Mikoa na nchi hizo. Fukwe zake ambazo zimehifadhiwa ni fursa pekee ya Ujenzi wa Hoteli za Kitalii kutokana na Watalii wengi kupenda kutembelea maeneo hayo. Hali kadhalika kuna samaki wa mapambo. Kubwa zaidi kunakadiriwa kuwepo kwa mafuta ya Petroli na Gesi, Utafiti bado unaendelea kufanywa na Kampuni ya Beach Petroleum kwa kushirikiana na TPDC Tanzania kubaini uwepo wa rasilimali hizo. Katika Ziwa hili ndiko inakopatikana Meli Kongwe kuliko Meli zote Duniani, Meli ya MV Liemba inakadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 100 huku bado ikiwa inafanya kazi.
 Fukwe za Ziwa Tanganyika kwa Mkoa wa Rukwa ni fursa pekee ambayo bado haijaharibiwa au kutumiwa vya kutosha. Ukanda huu ni kielelezo tosha cha mandhari na fursa nzuri za uwekezaji katika eneo hili ambalo kwa kiasi kikubwa linachochewa na ujenzi wa barabara za lami zinazoendelea kujengwa katika Mikoa hii itakayounganisha Mikoa hiyo na Ziwa Tanganyika pamoja na Nchi jirani zilizopakana na Ziwa hilo. 

 Baadhi ya makazi ya wananchi wanaozunguka Ziwa Tanganyika. Shughuli kubwa za wakazi hawa ni uvuvi na kilimo. Katika shughuli zao za uvuvi bado wanatumia zana duni ikiwepo mitumbwi ya mbao na nyambu zilizo chini ya kiwango. Fursa za uwekezaji kwenye eneo hili pia zinapatikana. Samaki wakuu wanaopatikana katika Ziwa hili wanaitwa Migebuka. Kuna Kampuni chache ambazo zimewekeza katika mradi huu na huuza bidhaa hiyo hadi nje ya nchi.
 Baadhi ya Hoteli zinazopatikana Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Nkasi katika Tarafa ya Kipili. Boti zinazoonekana ni kwa ajili ya wateja watakaohitaji kwenda kucruise ndani ya Ziwa. Bado yapo maeneo maalum ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hoteli za Kitalii katika ukanda huu.
 Mandhari ya Hoteli ya Kipili iliyopo Mkoani Rukwa
 Sehemu ya maegesho ya Boti kwa ajili ya wateja na watalii wanaotembelea ukanda huo hususani katika Hoteli ya Kipili.
 Hakika mandhari haya yanavutia na hivyo ni baadhi ya vyumba katika Hoteli hiyo ya Kipili.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya Kushoto na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana wakiwa wamejipumzisha katika moja ya maeneo ya mapumziko kwenye Hoteli ya Kipili baada ziara ya kuzungukia fukwe za Ziwa Tanganyika.

 Sehemu za maegesho ya Boti katika Hoteli ya Kipili.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana (Kushoto) wakiongea na watalii waliofikia katika Hoteli ya Kipili Wilayani Nkasi siku za hivi karibuni walipoenda kutembelea fukwe hizo.
Uwepo wa fukwe hizi ni fursa nzuri za ujenzi wa Hoteli za kitalii na shughuli nyingine zinazohusiana na uwekezaji na Utalii katika ukanda huu wa Ziwa Tanganyika. 
 Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Ally Kessy, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nkasi wakimaliza ziara ya kukagua Fukwe za Ziwa Tanganyika huku wakielekea kwenye Hoteli ya Kipili ambayo kwa kiasi kikubwa hupata wageni wa kitalii.
Vyumba vya Hoteli ya Kipili. Hoteli hii ipo katika ukingo wa Ziwa Tanganyika.
Sehemu kubwa ya Hoteli hii ya Kipili imeezekwa kwa makuti.
Watalii hutembelea ukanda huu. Kulia Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injiania Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana.

No comments:

Post a Comment