Monday, April 2, 2012

MAKABIDHIANO YA MKOA MPYA WA KATAVI YAFANYIKA JANA, WENGI WAJITOKEZA KUWALAKI VIONGOZI WAO WAPYA NA KUFURAHIA KUPATA MKOA MPYA

Safari ya kuelekea makabidhiano ilianza ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambaye alianza kwa kumuombea dua Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Rutegwe mapema kabla ya kuanza safari kuelekea Wilayani Mpanda Mkoa Mpya wa Katavi ambapo ndipo yalipofanyika makabidhiano hayo. Mkoa wa Rukwa umegawa na kuundwa Mkoa Mpya wa Katavi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kusogeza huduma zake kwa wananchi. Kwa pamoja viongozi wote wa Mikoa ya Rukwa na Katavi wameishukuru sana Serikali ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuugawa Mkoa wa Rukwa kwa maslahi ya wananchi wake.
Picha ya pamoja kati ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Rukwa na Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe mapema kabla ya kuaanza ya kuelekea makabidhiano ya Mkoa mpya wa Katavi yaliyofanyika Wilayani Mpanda Mkoa Mpya wa Katavi.

Mtu maarufu katika kabila la wasukuma ajulikanaye kwa jina la "Mchoma Simba" ambaye huveshwa mavazi hayo baada ya kuua Simba kama ishara ya ushujaa akicheza ngoma mbele ya uongozi wa Mikoa ya Rukwa na Mkoa Mpya wa Katavi kwenye makabidhiano ya Mkoa huo jana. Mkoa wa Rukwa umegawanywa na kuundwa Mkoa Mpya wa Katavi ikiwa ni jitahada za Serikali katika kusogeza huduma kwa wananchi wake. Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Joyce Mgana.
Mburudishaji huyo wa Kisukuma akiendelea kufanya vitu vyake

Baadhi ya watumishi kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa ikongozwa na Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Utawala na Rasilimali Watu Samson Mashalla, Afisa Tawala Festo Chonya na Kaimu Katibu wa Mkuu wa Mkoa Rukwa Frank Mateni wakiangalia burudani ya Mchezaji huyo wa Kisukuma.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akiwatambulisha baadhi ya viongozi waliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa Wananchi wa Wilaya ya Nkasi katika Kijiji cha Kizi waliokusanyika kumuaga Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe jana.

Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Rukwa ikiwa imejipanga tayari kushuhudia Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe (hayupi pichani) kwa baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa Mpya wa Katavi.
Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akisalimiana na Viongozi wa Chama na Serikali wa Mkoa Mpya wa Katavi waliojitokeza kumpokea baada ya kukabidhiwa kwao na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, kwa pamoja waliongozana kuelekea Katavi kwa ajili ya makabidhiano rasmi ya Mkoa huo Mpya wa Katavi.
Hapa ni Mpakani mwa Mikoa ya Rukwa na Katavi kwenye Mlima maarufu wa Lyamba Lyamfipa. Utawala wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya unaishia hapa, anashusha kibendera kuruhusu Utawala Mpaya wa Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe kupandisha bendera yake tayari kuipepeza kwenye Milima na Mabonde ya Utawala wake Mpya wa Mkoa Mpya wa Katavi. 

Bendera ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya imeshashushwa.
Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akiwa tayari kupepeza bendera yake kwa mara ya kwanza katika Mkoa wake mpya wa Katavi baada ya kukabidhiwa Mkoa huo jana. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia wananchi wa Mkoa Mpya wa Katavi waliojitokeza kwa wingi kabla ya kuwatambulisha viongozi wao katika uwanja wa Mpira wa Kashaulili uliopo Wilayani Mpanda. Aliwaomba wananchi hao kuwapa viongozi wao wapya ushirikiano wa dhati ili kurahisisha utendaji kazi wao kwa maendeleoa ya Katavi na Ukanda mzima wa Ziwa Tanganyika.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katikati akiwatambulisha viongozi wapya wa Mkoa Mpya wa Katavi kwa wananchi wa Mkoa huo jana kwenye uwanja wa Kashaulili Wilayani Mpanda katika makabidhianao ya Mkoa huo baada ya uliokuwa Mkoa wa Rukwa kugawanywa ikiwa ni jitihada za Serikali kusogeza huduma kwa Wananchi wake. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rajab Mtumwa Rutegwe na Katibu Tawala Injinia Emmanuel Kalobelo.
 Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akihutubia wananchi wake wa Mkoa Mpya wa Katavi mara baada ya kutambulishwa kwao na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Aliwaahidi ushirikiano wa hali na mali kuhakikisha Katavi inasonga mbele.
Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akiwa ameketi kwenye Kigoda akiombewa Dua ni Chifu wa Kabila la Wabende Chifu Victor Mfinula kabla ya kutunukiwa uchifu wa kabila hilo jana baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mkoa Mpya wa Katavi.

 Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akikabidhiwa uchifu wa kabila la wabende na Chifu wa Kabila hilo Victor Mfinula katika uwanja wa Kashaulili Wilayani Mpanda jana. Kushoto anayeshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akisoma taarifa yake ya makabidhiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe wakisaini makabrasha ya makabidhino ya Mkoa Mpya wa Katavi jana usiku katika Ikulu ndogo ya Katavi mara baada ya Mkoa wa Rukwa kugawanywa na kuundwa Mkoa Mpya wa Katavi ikiwa ni jitihada za Serikali kusogeza huduma kwa Wananchi wake. Hapo awali kabla ya kuteuliwa Dkt. Rutengwe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Katibu Tawala wa Mkoa Mpya wa Katavi Injinia Emmanuel Kalobelo wakisaini Nyaraka za Makabidhiano baada ya Mkoa wa Rukwa kumegwa na kuundwa Mkoa Mpya wa Katavi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kusogeza huduma kwa Wananchi wake.

Viongozi wa Dini nao walikuwepo kushuhudia makabidhiano hayo na kuyaombea dua pamoja na Sla kwa viongozi wa Makabidhiano hayo.
Katibu Tawala wa Mkoa Mpya wa Katavi, Injinia Emmanuel Kalobelo, Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na viongozi wengine wakiwa kwenye moja ya Sala zilizoongozwa na viongozi wa Dini waliohudhuria hafla hiyo.
Wananchi wengi wa Katavi walijitokeza kumlaki Kiongozi wao Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe na Katibu Tawala Mkoa huo Injinia Emmanuel Kalobelo.
Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mpya wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe, Injinia Emmanuel Kalobelo Katibu Tawala Mkoa wa Katavi na Alhaj Salum Mohammed Chima Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa wakifuatilia moja ya matukio katika hafla hiyo ya makabidhiano ya Mkoa Mpya wa Katavi.
Burudani ya Ngoma na Kwaya ilikuwepo kutumbuiza

No comments:

Post a Comment