Tuesday, April 3, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AFANYA MKUTANO NA VIONGOZI KATA ZA MAJENGO NA KATANDALA TAREHE 30 MACHI 2012, WANANCHI WATAKIWA KUCHANGIA UJENZI WA SHULE YAO YA KILIMANI MAWENI, ATAKAYEGOMA KUCHUKULIWA HATAUA ZA KISHERIA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya diwani wa Kata ya Katandala aliyesimama kushoto Mhe. Samuel Kisabwite alipokwenda kufanya mkutano na viongozi wa "WDC" Kata za Katandala na Majengo kujadili namna ya kupata fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Manispaa ya Sumbawanga ili wanafunzi waliofaulu waweze kwenda Shule. Katika Kikao hicho ilikubaliwa kuwa wenyeviti wa vijiji watakuwa mstari wa mbele katika kukusanya michango kutoka kwa wananchi wao na kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo la Serikali basi hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Malengo ni hadi kufikia Aprili mwaka huu vyumba vyote vinavyohitajika viwe vimeshakamilika na wanafunzi hao kuingia madarasani. Kulia ni diwani wa Kata ya Majengo Mhe. Faustina Vallery Kalyalya.
Afisa Mtendaji Kata ya Katandala akitoa taarifa ya Kata yake juu ya mchango wa kata yake katika ujenzi wa madarasa katika Shule ya Kilimani maweni. Katika Kata ya Katandala ni kaya 66 tu ndizo zilizochanga mchango wa shilingi 10,000/= kati ya Kaya 3750. Endapo kaya zote zitahamasika kuchanga zitapatikana shilingi milioni 37 na laki tano.
Kwa upande wa Kata ya Majengo ni Kaya 98 zimechanga kati ya kaya 3103 ambapo kama zitachanga kaya zote hizi itapatikana jumla ya Tsh Milioni 31 na thelethini alfu.  Wananchi wote wanahamasishwa kuchangia ili kuwezesha mradi huu kukamilika.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye kikao hicho, aliutaka uongozi wote wa kata kufanya kazi kuhakikisha lengo la Serikali kuinua sekta ya elimu linafikiwa. Alisema kwa kiongozi atayeshindwa kufanya hivyo basi hatakuwa pamoja naye na Uongozi wake utakuwa matatani kwa kushindwa kutimiza malengo ya uwepo wake madarakani.

Wajumbe wa kikao hicho ambao wengi wao ni Wenyeviti wa Mitaa katika kata za Katandala na Majengo

No comments:

Post a Comment