Saturday, April 28, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AWAOMBA WADAU WA MPANGO WA UZAZI SALAMA KUONGEZA NGUVU ZAIDI KUSAIDIA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO NCHINI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa Mashirika binafsi ya RFSU ya Sweden na taasisi ya RODI ya Mkoani Rukwa Ofisini kwake jana alipotembelewa na wadau hao ambao kwa pamoja wako Mkoani Rukwa katika kusadia mpango wa Uzazi Salama kwa afya ya Mama na Mtoto. Mkuu huyo wa Mkoa amezipongeza taasisi hizo kwa kazi nzuri wanazofanya na kuwaomba waongeze nguvu pamoja na kuzishawishi taasisi zingine na wafadhili waweze kusaidia kwenye mpango huo ambao ni muhimu kwa Afya ya Mama na Mtoto nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliamua kusimama na kujitambulisha kuwa yeye ni mdau mkubwa wa afya ya mama na mtoto katika mpango wa uzazi salama nchini, alifurahia ujio wa wageni hao kutoka Sweden Mkoani Rukwa na kusema kuwa ni faraja kubwa kwake yeye kama mdau kuona wafadhili hao wameamua pia kusaidia Rukwa. Wakwanza kushoto kwake ni Ndugu Mpina kutoka taasisi ya RODI, Olov Boggia wa RFSU ya Sweden na Agneta Falck RFSU kutoka Stockholm Sweden.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiendelea na mazungumzo na wadau hao (RODI ya Rukwa na RFSU ya Sweden) ambao walifika Ofisini kwake kujitambulisha kama wadau wa mpango wa uzazi salama nchini unaolenga usalama kwa mama na mtoto.

No comments:

Post a Comment