Friday, April 13, 2012

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KUTOKA MKOANI RUVUMA


Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Sehemu ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wafadhili Walter Reed, wanatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo:-
1.       PROGRAMME OFFICER:     NAFASI MOJA (1)
Kazi za kufanya:
·               Kusimamia na kuratibu shughuli za mpango wa Huduma kwa wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kwa kushirikiana na Mratibu wa Kudhibiti maambukizi ya UKIMWI Mkoa (Tiba)
·               Kutekeleza kazi nyingine kama atakavyoelekezwa na Msimamizi wa Huduma za Afya Mkoa
Sifa za kuingilia:
-            Wenye shahada ya Udaktari (MD) au Stashahada ya Udaktari   (AMO) ambaye amehitimu katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
-           Asiwe mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine ya Serikali na Serikali za Mitaa ndani ya Mkoa.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012 
2.        AFISA UFUATILIAJI NA TATHMINI (MONITORING & EVALUATION OFFICER 1 NAFASI MOJA (1)
Kazi za kufanya:
·         Kufuatilia na kutathmini maendeleo ya mradi kwa kushirikiana na Meneja wa Mradi
·         Kuwezesha na kutoa ushauri na tafsiri ya Sera, Mipango, mikakati na miongozo kuhusu taarifa za Afya kwa mujibu wa miongozo ya Wizara ya Afya
·         Kutekeleza kazi nyingine kama zitakavyoelekezwa na Meneja wa Mradi
Sifa za kuingilia:
-   Wenye Shahada/Shahada ya Uzamili katika fani ya Mipango, Uchumi na Takwimu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
-   Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
3.       MHASIBU:
Kazi za kufanya:
·                     Kufanya kazi kwa kushirikiana na Meneja wa Mradi
·                     Kusimamia shughuli zote za Uhasibu katika Mradi
·                     Kudhibiti hati za malipo
·                     Kujibu hoja za Ukaguzi
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
SIFA ZA KUINGILIA:
-            Awe na Shahada au Stashahada ya Uhasibu kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na Serikali

4.       WATUNZA KUMBUKUMBU NAFASI TANO (5)
Kazi za kufanya:
·         Kufanya kazi kwa mujibu wa maelekezo ya Meneja wa Mradi
·         Kuandaa na kutunza taarifa /kumbukumbu na nyaraka mbalimbali za Mradi
·         Kukusanya na kuhifadhi taarifa mbalimbali za wagonjwa.
Sifa za kuingilia:
-   Awe na Shahada au Stashahada, au cheti cha utunzaji wa kumbukumbu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali. 
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25/04/2012
Maombi yote yatumwe kwa: 

Katibu Tawala wa Mkoa,
S.L.P. 74,
SONGEA.
AU
                Mganga Mkuu wa Mkoa,
                S.L.P. 5,
                SONGEA.

No comments:

Post a Comment