Monday, May 7, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AFUNGUA MAFUNZO YA SIKU NNE YA UANDISHI WA HABARI ZA UCHUMI NA BIASHARA MKOANI RUKWA LEO

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na washiriki wa semina hiyo leo wakati akifungua mafunzo hayo rasmi yaliyoandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na kuratibiwa na Klabu ya Waandishi wa Habari ya Rukwa (Rukwa Press Club). Mafunzo hayo yatadumu kwa muda wa siku nne na jumla ya washiriki 18 kutoka vyombo vya habari tofauti vya Mikoa ya Rukwa na Katavi wanashiriki. Katika maneno yake ya ufunguzi Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka waandishi wa habari wa Rukwa kuhakikisha kuwa wanatumia nafasi yao vizuri kutangaza vivutio na fursa zinazopatikana Mkoani Rukwa kwa wadau ili kuvutia wawekezaji.
Muwezeshaji wa mafunzo hayo Ndugu Mnaku Mbali ambaye ni Muhariri wa gazeti la Business Times la jijini Dar es Salaam. Lengo kubwa la mafunzo hayo alisema ni kuwajengea uwezo zaidi waandishi wa Rukwa waweze kuandika habari za biashara na uchumi katika uelewa chanya kwa maendeleo ya jamii ya Rukwa na Taifa kwa ujumla.


Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Rukwa Peti Siyame akielezea changamoto wanazokabiliana nazo waandishi wa habari wa Mkoani Rukwa kwa Mkuu wa Mkoa huo leo. Changamoto kubwa aliyoisema ni ushirikishwaji hafifu wa waandishi wa habari katika shughuli za maendeleo jambo ambalo Mkuu huyo wa Mkoa alilitolea ufafanuzi kuwa alishaanza kulifanyia kazi hata wao wenyewe ni mashahidi.


Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya leo.

Katibu wa Rukwa Press Club Sami Jumaa Kisika akimtambulisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwenye mafunzo hayo leo.
Mkurugenzi na muendeshaji wa Blog ya Pembezoni Kabisa ambaye pia ni mwandishi wa gazeti la Mwanachi Mussa Mwangoka kulia na Joshua Joel wa ITV na Radio One wakifuatilia mafunzo hayo.
Muweka hazina wa Rukwa Press Club ambaye pia ni Mwandishi wa Habari wa Channel Ten na Magazeti mbalimbali Judy Ngonyani kushoto naye alikuwepo katika ufunguzi huo.
Baadhi ya washiriki wengine kutoka Rukwa na Katavi wanaoshiriki mafunzo hayo. Wapili kulia ni mdau Ernest Kibada kutoka Katavi. 
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa makini. Wapili kutoka kulia ni Gurian Adolph wa gazeti la Tanzania Daima na Radio Chemchem ya Wilayani Sumbawanga.

No comments:

Post a Comment