Sunday, May 6, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AANZISHA MPANGO WA RUKWA SALAMA UTAKAOHUSISHA UJENZI WA NYUMBA BORA ZA MAKAZI YA ASKARI POLISI MKAOANI HUMO JANA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa (RPC) Sunto Mantage wakiimba wimbo wa Utii wa Jeshi la Polisi kabla ya Mkuu huyo wa Mkoa kuzungumza na Polisi jana. Lengo la Mkuu huyo wa Mkoa kukutana na Jeshi hilo ilikuwa ni kujadili juu ya azma yake ya kuboresha makazi ya nyumba za Polisi Mkoani humo. Alisema kuwa kuna uhaba mkubwa wa nyumba za Polisi na hata zilizopo sio muafaka sana. Katika mpango huo maoni mbalimbali yalitolewa ikiwemo Polisi wenyewe kujitolea nguvu kazi kwa kufyatua matofali na michango kabla ya kuwashirikisha wadau wengine katika kuchangia zoezi hilo. Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa alionana na Waziri wa Mambo ya ndani na kumueleza tatizo lililopo ambapo aliahidi kutoa ushirikiano na Mkoa katika zoezi hilo. Katika kuhakikisha zoezi hilo linaaanza mara moja Injinia Manyanya alitoa ahadi ya kuchangia shilingi milioni 3.5. Alisema kuwa mapambao dhidi ya uhalifu na Rukwa kuwa salama hayawezekani bila Polisi wenyewe kuwa salama na kwamba hicho ndicho kilichomsuukuma kuanzisha mpango huo wa ujenzi wa makazi ya nyumba bora za Polisi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa jana ambapo alitangaza rasmi mpango wa Rukwa salama.  Katika mazungumzo hayo aliwataka askari wote kuwa na moyo wa kizalendo kwa kuipenda nchi yao na Serikali kwa ujumla. Aliwataka waache kasumba ya kuichukulia Serikali yote kuwa ni mafisadi pale mtu mmoja anapohusika na tukio hilo, kwani hata wao wenyewe kama Serikali wanapambana na ufisadi kwa maslahi ya nchi. Kuhusiana na mchakato wa mabadiliko ya katiba aliwataka Polisi washiriki kikamilifu katika mchakato huo kuhakikisha wanaingiza vipengele muhimu vinavyohusu jeshi hilo na kuondoa vile vyenye mapungufu. Pia aliwataka Polisi wazihamasishe familia zao na wao wenyewe washiriki katika zoezi lijalo la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika nchini kote tarehe 26 Agosti 2012.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akikabidhi jezi na mpira wa miguu kwa Sajenti Bahati Mtani kwa ajili ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa katika mpango wake wa kuhamasisha michezo Mkoani Rukwa. Sajenti Bahati alipokea vifaa hivyo kwa niaba ya kapteni wa timu ya hiyo ya Jeshi la Polisi ambaye hakuwepo. Anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa (RPC) Sunto Mantage.
Sajenti Bahati akionyesha vifaa hivyo kwa Wapiganaji wenzake. Alimshukuru Mkuu huyo wa Mkoa na kusema kuwa yeye ni Kiongozi wa mfano kwani hawajawahi kuona Mkuu wa Mkoa kuzungumza na Jeshi la Polisi hapo awali katika Mkoa wa Rukwa. 
Baadhi ya Askari Polisi walioshiriki katika Kikao hicho wakifuatilia kwa umakini majadiliano yaliyokuwa yakiendelea.


Askari wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo wao wa utii kazini.

No comments:

Post a Comment