Thursday, May 3, 2012

RAIS KIKWETE ATEUWA WABUNGE WATATU WAPYA LEO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wabunge watatu wapya kwa mujibu wa mamlaka ya uteuzi aliyo nayo chini ya Ibara ya 66(i) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge hao wapya ni Profesa Sospeter Muhongo, Bi. Janet Mbene na Bwana James Mbatia.

Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

3 Mei, 2012

No comments:

Post a Comment