Wednesday, May 2, 2012

SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI MEI MOSI ILIVYOFANA MKOANI RUKWA JANA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya wafanyakazi wakisubiri kupokea maandamano ya wafanyakazi katika uwanja wa Nelson Mandela katika Manispaa ya Sumbawanga jana kwenye sherehe ya Siku ya Wafanyakazi duniani. Mgeni Rasmi wa Sherehe hiyo alikuwa Mkuu huyo wa Mkoa, Kitaifa sherehe hiyo imefanyika Mkoani Tanga ambapo Rais Jakaya Kikwete alikuwa Mgeni Rasmi. Kaulimbiu ya sherehe hiyo mwaka huu ni "Mishahara duni, Kodi kubwa na Mfumuko wa bei Pigo kwa wafanyakazi" 

Maandamano yaliongozwa na vijana wa Skauti

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga

Mahakama

Energy Milling wakionyesha bidhaa zao za unga

Baraka Milling wakionyesha bidhaa yao za unga bora, Viwanda vyote hivi vipo Mkoani Rukwa

TTCL wakifanya onyesho lao la ufundi na utoaji huduma mkaoni Rukwa

Zimamoto wakifanya onyesho la kuzima moto

Maonyesho ya Sido

Wafanyakazi wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa wakionyesha mafunzo ya mfano kwa vitendo kwa mgonjwa wa Fistula katika sherehe za Meimosi zilizofanyika jana katika uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. Ujumbe uliobeba onyesho hilo ni kwamba ugonjwa wa Fistula unatibika na wagonjwa wanashauriwa kwenda katika vituo vya afya waweze kupata tiba. Kitaifa sherehe hizo zilifanyika Mkoani Tanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye alikuwa mgeni rasmi Injinia Stella Manyanya akiwa ameshikana mikono na viongozi waandamizi katika Serikali ya Mkoa wa Rukwa, watumishi na wananchi kwa ujumla wakiimba wimbo wa "Solidarity Forever" ambao ni wimbo maarufu wa nchini wenye kaulimbiu ya kuwaungaisha wafanyakazi katika kupata haki zao za msingi.

Watumishi wakiwa wanaimba wimbo huo kwa pamoja huku wakiwa wameshikana mikono.

Sehemu ya wananchi, Viongozi na Watumishi walishiriki sherehe hiyo ikiwemo sehemu ya jukwaa kuu katika uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa.

Wanafunzi nao walishiriki katika sherehe hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia wananchi na watumishi wa Mkoa wa Rukwa katika uwanja wa Nelson Mandela jana.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya aliyeshika kichanga cha mdoli akicheza ngoma na kikundi cha Kanondo kutoka katika Manispaa ya Sumbawanga jana kwenye uwanja wa Nelson Mandela katika sherehe za Siku ya wafanyakazi duniani (Meimosi) iliyofanyika kimkoa katika Manispaa ya Sumbawanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa huo, Kitaifa sherehe hizo zilifanyika Mkoani Tanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Mashindano ya kufukuza kuku kwa baadhi ya wastaafu yalipendezesha sherehe hizo

Afisa Tawala Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Festo Chonya akipokea zawadi ya cheti na Hundi yenye thamani ya shilingi laki tatu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Rukwa Injinia Stella Manyanya kama motisha kwake na wafanyakazi wengine waweze kujituma na kufanya kazi zaidi. 

Mchora Ramani Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Kevin Maundi akipokea zawadi ya ufanyakazi bora toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambayo ni Cheti na Cheki yenye thamani ya shilingi laki tatu kama motisha kwake na wafanyakazi wengine waweze kujituma na kufanya kazi zaidi.

Afisa Mifugo Respitch Maengo akipokea zawadi ya ufanyakazi bora ambayo ni Cheti na Cheki yenye thamani ya shilingi laki tatu na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.

Yudith Shimba Mhudumu bora katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa akipewa zawadi ya Cheti na Cheki yenye thamani ya Shilingi Laki tatu na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akikagua Timu za mpira wa miguu za Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na Manispaa ya Sumbawanga jana kwenye uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa kabla ya kuaza pambano kati yao ambalo lilikuwa sehemu ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani, timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga iliibuka mshindi wa bao 1-0 na kupewa zawadi ya shilingi Hamsini Alfu na Mpira wa Miguu wa ngozi uliotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa. Kitaifa sherehe hizo zilifanyika Mkoani Tanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Mtanange ukiwa unaendelea

Mpira wa pete ulikwa kati ya Polisi na Manispaa ya Sumbawanga

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa nasaha zake kwa timu zote mbili kabla ya kipindi cha pili baada ya mapumziko kuanza.

No comments:

Post a Comment