Monday, June 25, 2012

BE CAREFUL WITH THIS KIND OF MESSAGE. SIMILAR MESSAGES WERE USED TO STEAL PEOPLE'S PERSONAL INFORMATION. UNLESS YOU TRUST THE SENDER, DON'T CLICK LINKS OR REPLY WITH PERSONAL INFORMATION

FAST LOAN OFFER AT INTERNATIONAL LOAN COMPANY

AT INTERNATIONAL LOAN COMPANY LIMITED

AT INTERNATIONAL LOAN COMPANY WE RENDER AND LEND OUT TO THOSE WHO ARE FINANCIALLY DECLINED AND DISTRESS, ARE YOU TIRED IN ALL THE CHARGES BANKSHAVE BEEN IMPOSING ON YOU ALL THIS YEARS, OR YOU HAVE BEEN SCAMMED AND YOU NEED A RELIABLE AND CERTIFIED LENDING COMPANY WHO CAN GIVE YOU THE BESTTREATMENT AS TO GRANT YOU YOUR REQUEST, VISIT US TODAY:

LOANS OF DIFFERENT  CATEGORIES ARE BEEN OFFERED AS FOLLOWS:

1. NEED ASSISTANCE  FOR A BUSINESS LOAN
2. NEED FUND FOR FURTHER STUDIES
3. NEED FUND FOR TO IMPROVE YOUR FIRM OR INSTITUTION AS TO RAISE YOUR FIRM
4.FINANCIAL AID FOR MOOT GAGE
5. NEED FUND TO FOR INTERNET FACILITIES
6. CAPITAL TO FINANCE  PROJECT
5. SHIPING EQUIPMENT

NAME IT, WE ARE HERE FOR YOU TODAY, SO HURRY NOW AND GRAB THIS GREAT OFFER OF 4% INTEREST RATE AND THE REPAYMENT OF JUST 10-15 YEARS

FILL THE THE FOLLOWING IF YOU ARE CONCERNED AND CONTACT US
@ fastloancompany0@gmail.com

NAME .........

CITY.........

STATE ........

NATIONALITY.......

DATE OF BIRTH.....

PHONE NO....

COUNTRY....

BANK ACCOUNT DETAILS .........

AMOUNT NEEDED AS LOAN.........

SCANNED COPY OF DRIVER LISENCE,  INTERNATIONAL PASSPORT,  COLLATERAL IF ANY, AND  OTHER VITAL DOCUMENT FOR IDENTIFICATION.

MOVE ON TODAY AND GRAB THIS OFFER AS WE ARE TO MAKE LOAN WIRE TRANSFER TO YOUR BANK ACCOUNT WITHIN 24 HRS DELIVERY.

WE AWAIT YOU.

REGARDS,
MR. WILLIAM CHENG
LOAN DEPARTMENT

Friday, June 22, 2012

SERIKALI YAFANYA MABADILIKO MAKUBWA YA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NCHINI‏

Na Masoud Masasi, Dodoma

SERIKALI imefanya mabadiliko katika halmashauri hapa nchini kwa kuwateua wakurugenzi wapya 14 huku ikiwavua madaraka wengine nane ambao walionekana kushindwa kuwajibika ipasavyo katika halmashauri zao na kufanya ubadhirifu wa fedha za halmashauri zao. Pia katika mabadiliko hayo wakurugenzi kumi na moja wamepewa onyo kali huku wengine 22 wakihamishwa vituo vya kazi ambapo wakurugenzi watatu wakipumzishwa kufanya kazi katika halmashauri hizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ubadhilifu wa fedha . Akitangaza mabadiliko hayo mbele ya waandishi wa habari jana mjini Dodoma Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi)Hawa Ghasia alisema mabadiliko hayo yanatokana na kuboresha nidhamu na utendaji wa kazi kwa wakurugenzi hao.

‘’Wakurugenzi 14 wameteuliwa ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi huku wakurugenzi nane wakivuliwa madaraka hayo na Waziri Mkuu wengine watatu wakipumzishwa kabisa ambapo wakurugenzi 22 wakihamishwa katika vituo vyao na kupelekwa sehemu nyingine”

“Mabadiliko haya ni kuboresha utendaji wa kazi katika halmashauri zetu pamoja na kuongeza nidhamu na uwajibikaji wa kazi kwa wakurugenzi ambao walikuwa si waadilifu katika kutelekeza majukumu yao”alisema Ghasia.

Waziri huyo aliwataja wakurugenzi wapya walioteuliwa kuwa ni Jenifer Omollo ambaye anakuwa mkurugenzi wa Mji wa Kibaha,Fidelica MyovelaMkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Musoma na Khadija Maulid Makuwani ameteuliwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.

Aliwataja wengine kuwa ni Ibrahim Matovu ameteuliwa kuwa mkurugenzi halmashauri ya Muheza,Idd Mshili halmashauri ya Mtwara,Julius Madiga Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa yaMorogoro na Kiyungi Mohamedi Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Shinyanga.Wengini ni Lucas Mweri ameteuliwa Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Nanyumbu,Miriam Mmbaga halmashauri ya Kigoma,Mwamvua Mrindoko Mkurugenzi mtendaji Nachingwea,Pendo Malembeja Halmashauri ya Kwimba huku Pudenciana akiteuliwa mkurugenzi wa Ulanga.
Ruben Mfume Halmashauri ya Ruangwa na Tatu Selemani amekuwa mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kibaha ambapo waziri Ghasia alisema uteuzi huo ulifanyika april 24 mwaka huu.

Waziri huyo alisema wakurugenzi waliovuliwa madaraka kutokana na makosa mbalimbali katika Halmashauri zao kuwa ni Consolata Kamuhabwa(Karagwe),Ephraim Kalimalwendo(Kilosa),Elly Jesse Mlaki(Babati),Eustach Temu(Muheza),Jacob Kayange(Ngorongoro),Hamida Kikwega. (Chato),Majuto Mbuguyu(Tanga) na Raphael Mbunda halmashauri ya Manispaa ya Arusha.

Waziri Ghasia aliwataja wakurugenzi ambao wamepewa onyo kali kuwa ni Judetatheus Mboya(Newala),Lameck Masembejo(Masasi),Abdallah Njovu(Tandahimba),Jane Mutagurwa(Shinyanga),Silvia Siriwa(Aliyekuwa Mkurugenzi Manispaa ya Sumbawanga sasa Ileje),Kelvin Makonda(Bukombe),Alfred Luanda(Ulanga),Fanuel Senge(Tabora),Maurice Sapanjo(Chunya),na Beatrice Msomisi halmashauri ya Wilaya ya Bahi.

Pia waziri huyo alibainisha kuwa katika mabadiliko hayo wakurugenzi watatu ambao ni Xavier Tiweselekwa wa halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,Erica Mussica kutoka halmashauri ya Sengerema na Theonas Nyamhanga wamepumzishwa kufanya kazi katika halmashauri hizo. “Maamuzi haya yalifanyika katika kipindi cha mwaka 2011/12 na hawa waliopewa onyo walitendeka makosa yao katika halmashauri zao hivyo pia wakurugenzi 22 wamehamishwa katika vituo vyao vya kazi na kupangiwa sehemu nyingine ili waweze kuimarisha utendaji kazi wao”alisema. Alisema tayari wakurugenzi wanne waliotuhumiwa katika ubadhilifu mbalimbali katika halmashauri zao wameshafikishwa mahakamani huku wengine wakiendelea kufanyiwa uchunguzi ambapo amesema wakibainika watapelekwa mahakamani pia.

Alisema wale ambao walionekana hawakuhusika katika ubadhilifu katika vituo vyao vya kazi walipangiwa kazi nyingine huku wale walionekana utendaji wao sio mzuri walipumzishwa kabisa. Waziri huyo pia aliwataka wakurugenzi wapya walioteuliwa na wale wa zamani kuhakikisha wanafanya kazi kwa uhadilifu ili kuweza kuendelea kuboresha utendaji wa kazi katika mamlaka za serikali za mitaa nchini. Hata hivyo alisema hataweza kumchukulia hatua yoyote mkurugenzi kwa kusikia taarifa za mitaani na kuwataka wale wenye malalamiko kupeleka ushahidi kwake ambapo atafanya uchunguzi kabla ya mhusika kuchukuliwa hatua za kisheria.

‘’Tukisema tuanze kuchukuwa hatua kwa kusikia taarifa za mitaani basi tutajikuta tukifukuza wakurugenzi wote kinachotakiwa ni kuwa na ushahidi uletwe na utafanyiwa kazi na hatua zitachukuliwa kwa Yule atakayebainika”alisema waziri Ghasia.

UKWELI KUHUSU MISHAHARA YA WAHESHIMIWA WABUNGE

Wakati Bunge liko kwenye mchakato wa Bajeti ya 2012/13, yameanza kujitokeza maneno na taarifa mbalimbali juu ya kupanda kwa mishahara ya watumishi wa Umma wakiwemo Wabunge. Mathalani, siku ya Jumatano tarehe 20 Juni 2012, gazeti moja linatokalo kila siku lilikuwa na habari yenye kichwa kisemacho “Mishahara ya Wabunge juu”.
 
Ofisi ya Bunge imeona ni vyema kutoa ufafanuzi juu ya suala zima la mishahara ya Wabunge ili umma uweze kuelimika ipasavyo juu ya taratibu zinazotawala jambo hili kama ifuatavyo:
· Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo inajumuisha Fungu Na. 42 lenye Bajeti ya Bunge bado haijasomwa Bungeni, na hivyo haiwezekani leo hii kueleza kuwa kuna nyongeza ya bajeti inayohusu mishahara kwa Wabunge.
 
· Si kweli kwamba mishahara ya Wabunge imeongezwa toka kiwango wanacholipwa sasa, kwa kuwa mishahara yao kama ilivyo ya watumishi wote wa umma, hurekebishwa kwa waraka maalum toka Ofisi ya Rais, na si Kamisheni au Kamati yoyote ya Bunge.
· Waraka wa mwisho wa toka Ofisi ya Rais unaotoa Masharti ya Kazi ya Mbunge ulitolewa tarehe 25 Oktoba 2010, na kueleza kuwa Mbunge atalipwa mshahara katika ngazi ya LSS (P) 2, na ni waraka huo unaotumika mpaka sasa.
 
· Mapendekezo ya ongezeko la 32% ya Bajeti ya Ofisi ya Bunge yaliyooneshwa kwenye kitabu cha Bajeti namba 2, cha matumizi ya kawaida yaliyowasilishwa mezani ni ya matumizi mengine ambayo hayana uhusiano na ongezeko la mishahara.
 
Mwisho, Ofisi ya Bunge wakati wote inathamini sana mchango wa vyombo vya habari katika juhudi za kuelimisha umma juu ya kazi za chombo chao cha uwakilishi. Hata hivyo, Ofisi inasikitishwa sana na habari za upotoshaji zinazotolewa kwa lengo la kujenga chuki kati ya Wabunge na watu wanao wawakilisha.
 
Kwa mantiki hiyo, tunazidi kuwasihi Waandishi waandike habari au makala baada ya kufanya utafiti wa kina kuhusu jambo husika na pale inapobidi waweze kupata ufafanuzi toka Idara husika katika Ofisi ya Bunge, ili kuepuka kuupotosha umma.
 
 
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941, DODOMA.
21 Juni 2012

Thursday, June 14, 2012

WAZIRI WA FEDHA AWASILISHA BUNGENI BAJETI YA MWAKA 2012/13

Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa akionyesha mkoba wenye hotuba ya bajeti ya mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2012/13 leo mjini Dodoma kabla ya kuwasilisha.
Wapiga picha wakigombea picha ya Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa wakati aliponyanyua mkoaba wa Bajeti ya Serikali ya 2012/13, Bungeni Mjini Dodoma Juni 14, 2012.
Waziri wa Fedha,Dkt.William Mgimwa akiongozwa na Mpambe wa Bunge kuingia Bungeni kusoma Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2012/13, Mjini Dodoma Juni 14
Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa akisoma bajeti ya Serikali ya 2012/13, Bungeni Mjini Dodoma Juni 14, 2012
Mabalozi wa Nchi mbalimbali waliohudhuria Bungeni kusikiliza Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2012/13 iliyosomwa na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa, Bungeni Mjini Dodoma Juni 14,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
KUSOMA HOTUBA NZIMA BOFYA READ MORE CHINI KUSHOTO.

Monday, June 11, 2012

WAZIRI WA HABARI AZUNGUMZA NA MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO WA SERIKALI JIJINI MWANZA LEO


Waziri wa Habari, vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali leo jijini Mwanza.Pamoja na mambo mengine amewataka maafisa hao kuielimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo yanayofanywa na serikali kupitia vyombo vya habari.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda (mstari wa kwanza) akifuatilia mada kuhusu changamoto zinazoikabili Tanzania katika kuhama kutoka mfumo wa Analojia kwenda Digitali kufikia mwaka 2012 katika Kikao kazi cha Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali leo jijini Mwanza. Wengine wanaoonekana nyuma ni maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali.
 
Waziri wa Habari, Vijana na Utamaduni Dkt. Fenella Mukangara (mstari wa kwanza katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara hiyo na maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali mara baada ya kufungua kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano leo jijini Mwanza. Nyuma yake ni Afisa Habari Mkoa wa Rukwa Hamza Temba. Picha na Aaron Msigwa-Maelezo.

Friday, June 8, 2012

VIJIMAMBO YA WAZIRI MKUU WA UHOLANZI (NETHERLANDS)


Waziri Mkuu wa Uholanzi, Mhe. Mark Mutte akirejea nyumbani kwake toka kazini kwa kutumia usafiri wa baiskeli huku akimiminiwa saluti na walinzi wake. Hii hapa kwetu vipi?

Thursday, June 7, 2012

WAFANYAKAZI OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA WAJIMWAGA KWENYE USAFI WA MAZINGIARA LEO KAMA KAWA KWENYE ALHAMISI YA KILA WIKI

Kila siku ya Alhamisi ya kila wiki wafanyakazi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa hujumuika kwenye usafi wa mazingira ya Ofisi zao na maeneo ya jirani. Katika usafi wa leo Alhamisi tarehe 07/06/2012 kazi kubwa iliyofanyika ni kufagia, kuchoma taka ngumu moto, na kufyeka nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo. Mkuu wa Mkoa wa huo Injinia Stella Manyanya hujumuika na wafanyakzi wote kwenye usafi huo japo siku ya leo hakuwepo kutokana na kuwepo safarini kwa majukumu mengine muhimu ya kikazi.

BABA NA MWANA

Ni mara chache sana kuwakuta kina baba wakiafrika wakiwa wamewabeba watoto zao mgongoni kama alivyofanya baba huyu wa Mkoa wa Rukwa alipokutwa na Kamera yetu leo asubuhi akikatiza maeneo ya jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo. Jina lake halikuweza kufahamika mara moja. Huu ni mfano wa kuigwa wa mapenzi ambayo kina baba wanatakiwa kuwa nayo kwa familia zao haswa watoto zao na sio tu kuwaachia kina mama kufanya kazi za kuhudumia na kulelea watoto. 

Wednesday, June 6, 2012

TANGAZO KWA UMMA / PUBLIC NOTICE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MKOA WA RUKWA
Anwani ya Simu: “REGCOM”
SIMU:(025)-2802137, 2802138,2802187
FAX NA. (025) 2802217  
    
          
OFISI YA MKUU WA     MKOA
 S.L.P. 128,
 SUMBAWANGA.


           
TANGAZO KWA UMMA
UPOTEVU WA VITABU ISHIRINI (20) VYA LESENI ZA BIASHARA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa inapenda kuutangazia Umma kuwa imepotelewa na vitabu ishirini (20) vya leseni za biashara vilivyopotea tarehe 22 Mei 2012 katika moja ya Daladala Jijini Dar es Salaam.
Vitabu hivyo vilivyotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara vikiwa na  kumbukumbu namba 1389501 mpaka 1391500.
Kwa yeyote atakayeona vitabu hivyo au kuvinunua anaombwa avipeleke kituo chochote cha polisi kilicho karibu yake au kutoa taarifa juu ya mwenye navyo katika kituo hicho.
Ifahamike kuwa vitabu hivyo ni batili hivyo haviruhusiwi kutumika kwa namna yeyote ile. Na atakayethibitika kuvitumia atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.
Ewe mfanyabiashara, epuka manunuzi na matumizi ya vitabu vyenye namba tajwa hapo juu kwa usalama wa biashara yako.
Kwa mawasiliano tunaomba mtumie namba zetu hapo juu.
Tunaomba ushirikiano wenu.
IMETOLEWA NA
KATIBU TAWALA MKOA
RUKWA
07/06/2012

KAMERA YA RUKWAREVIEW KATIKA BAADHI YA MITAA YA MJI WA SUMBAWANGA JIONI YA LEO, "SUMBAWANGA NG'ARA" YALETA MABADILIKO YA USAFI KATIKA MJI HUU

Monday, June 4, 2012

HEALTH CORNER: THE SEVEN DANGEROUS

DON 'T ACT THE 7 ACTIONS BELOW AFTER YOU HAVE A MEAL  

* Don't smoke- Experiment from experts proves that smoking a cigarette after meal is comparable to smoking 10 cigarettes (chances of cancer is higher).
* Don't eat fruits immediately - Immediately eating fruits after meals will cause stomach to be bloated with air. Therefore take fruit 1-2 hr after meal or 1hr before meal.    
* Don't drink tea - Because tea leaves contain a high content of acid. This substance will cause the Protein content in the food we consume to be hardened thus difficult to digest.

* Don't loosen your belt - Loosening the belt after a meal will easily cause the intestine to be twisted & blocked.
* Don't bathe - Bathing after meal will cause the increase of blood flow to the hands, legs & body thus the amount of blood around the stomach will therefore decrease. This will weaken the digestive system in our stomach. 
      
 
* Don't walk about - People always say that after a meal walk a hundred steps and you will live till 99. In actual fact this is not true. Walking will cause the digestive system to be unable to absorb the nutrition from the food we intake.    
               

* Don't sleep immediately - The food we intake will not be able to digest properly. Thus will lead to gastric & infection in our intestine.
  
FINALLY DONT JUST KEEP THIS MESSAGE  . ..
PLEASE TELL YOUR
FRIENDS. LET THEM BE AWARE!! !

Sunday, June 3, 2012

HATA RAIS WETU NAE HUSHIRIKI KWENYE MAZOEZI KULINDA AFYA YAKE, WEWE JE?

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, aliye katika mapumziko mafupi jijini Arusha, akiwa katika mazoezi yake ya kutembea kilomita tatu kila asubuhi na jioni kabla ya kufanya mazoezi ya viungo na kuingia gym, katika kuuweka mwili wake katika hali ya ukakamavu na afya. Wakaazi wengi wa Arusha ambao wamemuona akitembea wamesisimkwa na kufurahishwa sana na hatua hiyo ya kiongozi mkuu wa nchi kuwa mstari wa mbele katika kujenga afya kwa mazoezi ya kila siku, na kutaka kila mtu, si viongozi tu, kuiga mfano wake.
PICHA NA IKULU