Wednesday, June 6, 2012

TANGAZO KWA UMMA / PUBLIC NOTICE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MKOA WA RUKWA
Anwani ya Simu: “REGCOM”
SIMU:(025)-2802137, 2802138,2802187
FAX NA. (025) 2802217  
    
          
OFISI YA MKUU WA     MKOA
 S.L.P. 128,
 SUMBAWANGA.


           
TANGAZO KWA UMMA
UPOTEVU WA VITABU ISHIRINI (20) VYA LESENI ZA BIASHARA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa inapenda kuutangazia Umma kuwa imepotelewa na vitabu ishirini (20) vya leseni za biashara vilivyopotea tarehe 22 Mei 2012 katika moja ya Daladala Jijini Dar es Salaam.
Vitabu hivyo vilivyotolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara vikiwa na  kumbukumbu namba 1389501 mpaka 1391500.
Kwa yeyote atakayeona vitabu hivyo au kuvinunua anaombwa avipeleke kituo chochote cha polisi kilicho karibu yake au kutoa taarifa juu ya mwenye navyo katika kituo hicho.
Ifahamike kuwa vitabu hivyo ni batili hivyo haviruhusiwi kutumika kwa namna yeyote ile. Na atakayethibitika kuvitumia atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria zilizowekwa.
Ewe mfanyabiashara, epuka manunuzi na matumizi ya vitabu vyenye namba tajwa hapo juu kwa usalama wa biashara yako.
Kwa mawasiliano tunaomba mtumie namba zetu hapo juu.
Tunaomba ushirikiano wenu.
IMETOLEWA NA
KATIBU TAWALA MKOA
RUKWA
07/06/2012

No comments:

Post a Comment