Thursday, June 7, 2012

WAFANYAKAZI OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA WAJIMWAGA KWENYE USAFI WA MAZINGIARA LEO KAMA KAWA KWENYE ALHAMISI YA KILA WIKI

Kila siku ya Alhamisi ya kila wiki wafanyakazi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa hujumuika kwenye usafi wa mazingira ya Ofisi zao na maeneo ya jirani. Katika usafi wa leo Alhamisi tarehe 07/06/2012 kazi kubwa iliyofanyika ni kufagia, kuchoma taka ngumu moto, na kufyeka nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo. Mkuu wa Mkoa wa huo Injinia Stella Manyanya hujumuika na wafanyakzi wote kwenye usafi huo japo siku ya leo hakuwepo kutokana na kuwepo safarini kwa majukumu mengine muhimu ya kikazi.

No comments:

Post a Comment