Sunday, September 30, 2012

MATUKIO YA WAZIRI MKUU WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda ambaye ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM akifungua mkutano mkuu wa Uchaguzi wa CCM wilaya za Mlele na Mpanda mkoani Katavi kwenye Shule ya Sekondari ya Wazazi ya Milala wilayani Mpanda, Septemba 30,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazamo shimo lililochimbika kwenye makutano ya barabara ya Bugwe na ya Soko Kuu mjini Mpanda Septemba 29, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Friday, September 28, 2012

WAFUGAJI NA WAFANYABIASHARA WA MAZAO MKOANI RUKWA WAASWA KUTUMIA BANK BADALA YA KUHIFADHI FEDHA ZAO SEHEMU ZISIZO RASMI

Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya akipokea sarafu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru Tanzania bara kutoka Mkurugenzi wa benki kuu kanda Mbeya, Moses Kasabile ambayo ina thamani ya Sh 50,000 kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Rukwa jana ofisini kwake mjini Sumbawanga.
 
Meneja wa Idara ya uchumi wa Benki kuu kanda ya Mbeya, Allan Tuni akizungumza katika kikao baina ya viongozi wa benki kuu kanda ya Mbeya na uongozi wa mkoa wa Rukwa jana ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa.
 
-------------------------------------
Mussa Mwangoka, Sumbawanga-Rukwa Yetu

WAFUGAJI na wafanyabiashara wa mazao mkoani Rukwa, wametakiwa kuachana na tabia iliyojengeka miongoni mwao ya kuhifadhi fedha kwenye viroba na ngozi na badala yake wajenge utamaduni wa kuweka fedha hizo benki.

Meneja wa Idara ya Uchumi wa Benki kuu kanda ya Mbeya, Allan Tuni alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye kikao baina viongozi kutoka benki hiyo na uongozi wa mkoa wa Rukwa kilichofanyika ofisi ya mkuu wa mkoa huo.

Alisema kuwa kuweka fedha benki kuna faida nyingi zikiwamo kuwapo kwa bima inayowalinda waekaji na haki zao, hivyo hakuna sababu za msingi za kuwafanya wafanyabiashara kuogopa kuweka fedha zao kwenye taasisi hizo.

"kuna taarifa kuwa huku kuna wafugaji wengi ambao wanahifadhi fedha kwenye viroba na ngozi, sasa waache kufanya hivyo na waanze utamaduni wa kuweka pesa benki kwani hali hiyo itasaidia watu wengine waweze kupata mikopo kutoka kwenye taasisi hizo kifedha hali ambayo itasaidia fedha nyingi kuingia mzunguko' alisema.

Awali, Mkurugenzi wa benki hiyo kanda ya Mbeya, Moses Gasabile alisema kuwa wapo kwenye hatua za mwisho za kufungua kituo cha benki hiyo mkoani Rukwa ili wateja wao ambao ni taasisi za kifedha zilizopo mkoani Rukwa na Katavi wasiangaike tena kuzifuata fedha Mbeya kama ilivyo sasa.

Mkurugenzi Gasabile alisema kuwa licha kutumia gharama kuzifuata fedha Mbeya lakini tatizo jingine linalojitokeza ni kutorudhishwa kwa fedha za noti na sarafu chakavu kutokana na umbali uliopo hali ambayo inasababisha kuadimika kwa sarafu hivyo uwepo wa kituo hicho mkoani humo kumaliza tatizo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya alisema kuwa ipo haja ya kufikia mahali kwamba kilimo chetu kitoe thamani ya kazi inayofanywa na wananchi.

Alisema kuwa ikiwezekana katika kudai wanazuia mfumuko wa bei, benki hiyo itoe fedha ya kutosha ili kununua chakula kwa wakulima wa mkoa huo kwa bei inayostahili badala ya kununua nje ya nchi tena kwa bei kubwa zaidi kwani kufanya hivyo ni kutowatendea haki wakulima.

Tuesday, September 25, 2012

BARABARA ZA LAMI ZINAZOENDLEA KUJENGWA KWA KASI MKOANI RUKWA TUMAINI JIPYA KWA WANANCHI WA MKOA HUO

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi waliokutwa na Kamera yetu wakifurahia ujio wa barabara za lami zinazoendelea kujengwa Mkoani Rukwa zikiunganisha Mkoa huo na Mikoa ya Mbeya na Katavi.
 

Baadhi ya wakandarasi wanaojenga barabara ya Laela-Sumbawanga wakiwa kazini. Kwa sasa kasi ya ujenzi wa barabara za Tunduma-Ikana, Ikana-Laela, Laela-Sumbawanga, na Sumbawanga-Kasanga imeongezeka ikilinganishwa na hapo awali.
 


Monday, September 24, 2012

TIMU YA MPIRA WA MIGUU (RAS RUKWA) YAWASILI MKOANI MOROGORO KUSHIRIKI MASHINDANO YA SHIMIWI 2012

Muda mfupi baada ya kungia Mkoani hapo, Mikakati ya Ushindi na Malazi ikaanza kufanyiwa kazi. Katibu wa Tibu (Ras Rukwa Sports Club) Joseph Chambala akizungumza na baadhi ya wachezaji.
 
Robani wa Timu (Dereva Moses Ngajiro) akishusha mizigo. 
 
Utafutaji wa Malazi ukiendelea. Kulia ni Kocha wa timu hiyo Godfrey Mwiga na Dkt. Lasway daktari wa Timu. Katikati ni kapteni wa timu Dkt. Marwa.
 
Safari ilikuwa tete kwani jumla ya wachezaji na viongozi 18 walipanda gari moja aina ya Land Cruiser Hard Top. Hakika hii ilikuwa ni zoezi tosha.

BREAKING NEWSSSSSSSSSSS........ASKOFU MKUU ANGLIKANA DK. MOKIWA ANUSURIKA KUPATA KIPIGO KUTOKA KWA WAUMINI WAKE MKOANI RUKWA, AOKOLEWA NA POLISI.


Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Valentino Mokiwa aliyevuliwa kofia ya kiaskofu akiwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia wakimtoa nje ya Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga baada ya kuzuka kwa vuguru kubwa jana.
 
Mmoja wa waumini wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote la mjini Sumbawanga akiwa na jazba wakati wa vurugu zilizoibuka jana mara baada ya kutolewa uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulizi wa polisi. picha na Mussa Mwangoka
Waumini wa Kanisa la Anglikana la watakatifu wote mjini Sumbawanga jana wakipiga kelele kupinga uamuzi wa nyumba ya maaskofu wa kuridhia askofu Mathayo Kasagara kuwa kiongozi wao ambapo vurugu kubwa zilizuka na kusababisha askofu Mkuu wa kanisa hilo Dk Mokiwa kuondolewa akiwa chini ya ulizi wa polisi.

Na Mussa Mwangoka-Sumbawanga
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania la Dk. Valentino Mkowa jana amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kunusurika kupata kipigo kutoka kwa waumini wake waliokuwa wenye hasira kali.

Vurugu kubwa ziliibuka mara baada ya kusomwa kwa tamko lililothibisha kuwa nyumba ya maaskofu inamtambua Askofu Canon Kasagara kuwa ni kiongozi wao halali wa kanisa la Anglikana la watakatifu wote Jimbo la Ziwa Rukwa mjini Sumbawanga.

Katibu mkuu wa Anglikana Dk, Dickson Chilongani ndiye aliyesoma tamko hilo mara baada ya kumalizika kwa ibada iliyoongozwa na Askofu Mkuu Dk. Mokiwa.

Akisoma tamko hilo Katibu Mkuu alisema kuwa sehemu ya hoja za msingi kamati ya usimamizi wa kanisa hilo zilidai kuwa uchaguzi uliomweka madarakani Askofu Kasagara uligubikwa na rushwa,si za kweli na nyumba ya maaskofu imeshindwa kuthibitisha hilo hivyo Kasagara ni askofu wao halali.

Kutokana na kauli hiyo waumini hao, walianza kupiga kelele ya kupinga maelezo hayo hali iliyosababisha mjumbe wa Kamati ya kusimamia kanisa hilo Flugence Lusunzu aliposhika kinasa sauti na kueleza kuwa wanao ushahidi wa kutosha kuwa rushwa ilitumika kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi huo uliofanyika zaidi ya miaka miwili iliyopita.

Alidai kuwa uamuzi wa nyumba ya maaskofu haukuwapa fursa ya kusikiliza upande wa walalamikaji ili hali ushahidi upo wazi, kutokana kauli hiyo zilianza fujo zilisababisha askofu Mokiwa kutolewa lugha chafu, kuvuliwa kufia yake ya kiaskofu, huku wengine warusha viti ambavyo alivikwepa hado alipoondolewa akiwa chini ya polisi waliokuwa wamevalia kiraia.

Hali hiyo iliharibu amani iliyokuwa imetawala ndani ya Kanisa hilo ambapo uligeuka kuwa uwanja wa vita huku waumini wakisikika wakidai kuwa ni heri kanisa hilo lifungwe kuliko Askofu Kasagara kuliongoza.

Awali tangu nyakati za asubuhi, polisi waliovaa kiraia walitanda katika viunga vya kanisa hilo ambapo Askofu Mokiwa aliwasili na kurakiwa vizuri na waumini wake waliokuwa wakishangilia kwa nyimbo na mapambio.

Hata hivyo tayari waumini wa Kanisa hilo walionya kwamba askofu Kasagara asikanyage kwenye eneo hilo, kwani kufanya hivyo kunge hatarisha amani onyo ambalo upande wa askofu Kasagara walitii hivyo askofu huyo mwenye makazi yake wilayani Mpanda alibaki katika nyumba moja ya kulala wageni alikokuwa amefikia.

Mmoja wa waumini Julius Michael alisema kwa kuwa waumini wa Jimbo la Rukwa hawamtaki askofu Kasagara hakuna sababu ya kuwalazimishwa lakini nyumba ya maaskofu inapaswa kuangalia uwezekano wa kuligawa jimbo hilo.

Tayari Serikali imegawa mkoa wa Rukwa na kuzaa ule wa Katavi sasa hakuna umuhimu wa kuwalazimisha waumini wampokee mtu wasiyemtaka nyumba ya maaskofu waanzishe jimbo katika mkoa huo mpya na aongoze Kasagara.

Alisema iwapo watatumia nguvu kumuweka Askofu huyo Rukwa haitasaidia kitu kwani hawezi kuwaongoza watu wasiotaka kushirikiana nae.

Mgogoro katika Kanisa hilo umedumu kwa zaidi ya miaka miwili sasa ambapo siku za nyuma waumini hao walimzuia Askofu Mkuu, Dk Valentino Mkowa kumsimika Askofu huyo na badala yake alisikimkwa tarehe 16, Juni mwaka jana Mjini Mpanda.

Kutokana na kujitokeza kwa mgogoro huo, ilifunguliwa kesi mahakamani ya Hakimu Mkazi Sumbawanga na waumini wa anglikana, Fulgence Rusunzu na Rojas Bendera na wenzao 191 yenye namba 11/2011 wakipinga kuchaguliwa kwa askofu Kasagala kuwa kiongozi wa Dayosisi hiyo.

Ambayo iliondolewa baada ya pande mbili zinazovutana kukubaliana kuwa baraza la maaskofu ndilo lenye dhamana ya kutatua mgogoro huo. Mwisho.

Thursday, September 20, 2012

MWENGE WA UHURU WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA

Mwenge wa Uhuru ukipewa heshma ya mwisho kwa stali ya mchakamchaka kabla ya kukabidhiwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi mara baada ya kumaliza mbio zake mkoani humo jana, Wakijumuika kwenye gwaride hilo la utii kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddy Kimanta, Kiongozi wa Mwenge Kitaifa Capt. Honest Mwanossa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya. Jumla ya miradi 27 iliyogharimu zaidi ya bilioni 5 ilizinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi katika Mkoa wa Rukwa.
 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada ya kumaliza mbio zake Mkoani Rukwa ambapo Jumla ya miradi 27 iliyogharimu zaidi ya bilioni 5 ilizinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi katika Mkoa wa Rukwa.

 Baadhi ya wananchi Mkoani Rukwa waking'ang'ania kushika mwenge wa uhuru kabla ya Mwenge huo kuondoka kuelekea kuanza mbio zake Mkoani Katavi hapo jana.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nkasi wakiwa wamebeba bango lililokuwa na ujumbe wa Mwenge wa Uhuru. Ujumbe wa Mwenge wa mwaka huu kitaifa ni Mabadiliko ya Katiba Timiza Wajibu Toa Maoni yako na Mapambano dhidi ya Ukimwi na Dawa za kulevya.
 
Muongozaji wa Blog ya Rukwareview Mr. Temba (shoto) akishare Photo na Mkimbiza Mwenge kitaifa Ndugu Kajia Godfrey kutoka Shinyanga kabla ya kumaliza mbio hizo Mkoani Rukwa jana. 
 
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Capt. Honest Erenest Mwanossa akiagana na viongozi wa Mkoa wa Rukwa mara baada ya kukamilisha jukumu zito la kukimbiza mwenge katika Wilaya tatu za Mkoa wa Rukwa ambazo ni Sumbawanga, Kalambo na Nkasi. Alieshikana nae mkono na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla.
 
Wananchi wengi wa Mkoa wa Rukwa walihasika kuulaki Mwenge huo wa Uhuru kwani wengine walilazimika kuhatarisha maisha yao kwa kupanda juu ya miti ili waweze kuuona Mwenge huo.
 

VIDEO YA MKUU WA MKOA WA RUKWA AKISAKATA RUMBA NA MADEREVA WA BODABODA KUUKARIBISHA MWENGE WA UHURU KATIKA UWANJA WA NDEGE WA SUMBAWANGA


Saturday, September 15, 2012

MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOANI RUKWA LEO NA KUANZA MBIO ZAKE ZA UHAMASISHAJI WA MAENDELEO

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya akiwasalimu wananchi wa Mkoa wa Rukwa waliojitokeza katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga kwa ajili ya kuupokea mwenge wa uhuru ambao umemaliza mbio zake Mkoani Kigoma na kuwasili Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufanya mbio zake katika Wilaya tatu za Sumbawanga, Kalambo na Nkasi kwa muda wa siku nne.
 
Kiongozi wa mwenge kitaifa mwaka 2012 Kapteni Honest Ernest Mwanossa akiwa na wenzake pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakifanya maandalizi ya kuukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Sumbawanga leo.
 
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Rukwa kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Samson Mashalla, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi na RPC wakishuhudia mapokezi hayo.
 
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mathew Sedoyyeka akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya tayari kwa kuanza mbio zake katika wilaya hiyo ambapo baadae utaenda Wilaya ya Kalambo na kumalizia katika Wilaya ya Nkasi.

Viongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa wakiwa na viongozi wa Wilaya ya Sumbawanga wakikimbiza mwenge katika moja ya barabara za Manispaa hiyo ikiwa ni kuunga Mkono na kukagua mradi wa Sumbawanga Ng'ara ambao lengo lake kuu ni kudumisha usafi katika Mji wa Sumbawanga. Mradi huo umeasisiwa na Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya na kuzinduliwa rasmi na Mhe. Makamu wa Rais Mohammed Gharib Billal alipokuwa ziarani Mkoani Rukwa.
 
Kiongozi wa mwenge kitaifa mwaka 2012 Kapteni Honest Ernest Mwanossa akipandikiza Samaki katika bwawa la kufugia Samaki lililopo Mishamo katika Manispaa ya Sumbawanga alipofika kukagua ufugaji wa samaki. Nyuma yake ni waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kutafuta taswira mwanana kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa wananchi.
 
Kiongozi wa Mbio za mwenge kitaifa akiwa anazungumza na wananchi wa Mkoa wa Rukwa. Alisema kuwa Mwenge wa Uhuru lengo lake kubwa ni kuhamasisha miradi ya maendeleo pamoja na kuubiri amani na mshikamano ambao ndio nguzo kubwa ya mafanikio ya nchi ya Tanzania. Alisema wale wote wanaoipiga vita Serikali iliyopo madarakani hawaitendei haki kwani maendeleo yote yaliyoletwa nayo ikiwemo barabara na mashule wanazitumia wote bila kujali dini zao au vyma vyao. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwapa utaratibu wa waendesha Pikipiki (Bodaboda) namna ya kupokea Mwenge wa Uhuru. Jumla ya waendesha Pikipiki 100 walishirikishwa katika mapokezi ya Mwenge huo wa Uhuru.
 
Vikundi vya ngoma vilikuwepo kutoa burudani.
 
Kwenye baadhi ya uzinduzi wa miradi baadhi ya wananchi walilazimika kupanda juu ya miti ili kuona matukio yote bila chenga.
 

Thursday, September 13, 2012

WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI YAFANYA MKUTANO WA UANZISHWAJI WA ENEO HURU NA MAGONJWA YA MIFUGO KATIKA MKOA WA RUKWA

Picha ya pamoja kati ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang'a na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Winston Mleche pamoja na wataalamu wa Mifugo kutoka Mikoa ya Rukwa, Njombe, Katavi, Tabora, Mbeya, Singida, Shinyanga, Mwanza, Kigoma, Iringa, Kagera, Mara, Simiyu na Geita katika kikao kilichowashirikisha wataalamu hao katika kujadili mpango wa kuanzishwa eneo huru la magonjwa ya mifugo katika Wilaya za Sumbawanga na Nkasi Mkoani Rukwa kwa lengo la kuwezesha kufanyika kwa biashara ya mifugo na mazao ya mifugo kwa kufuata vigezo na masharti ya kimataifa. 
 
 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambae pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla akiwakaribisha wageni hao Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufanya mkutano huo muhimu kwa maendeleo ya sekta ya mifugo mkoani Rukwa na Taifani kwa ujumla.

 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Moshi Chang'a ambae pia ni Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kalambo akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya ambaye yupo safarini kikazi. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Winston Mleche ambae pia ni Mkurugenzi wa huduma za mifugo nchini. Katika hotuba yake hiyo alielezea changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi ikiwemo uimarishaji wa mifumo ya usafirishaji, uchukuzi na mawasiliano, kuboresha miundombinu ya masoko ya mifugo, kuendelea kuboresha aina ya mifugo na mifumo ya uzalishaji mifugo, kuboresha taratibu za umiliki wa ardhi na kuzuia magonjwa mbalimbali ya mifugo. Hata hivo Mkoa wa Rukwa umepiga hatua kubwa katika kupambana na magonjwa hatarishi ya mifugo ambayo kwa sasa yapo kwa kiwango kidogo sana. 
 
 Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa kitengo cha Uchumi na Uzalishaji Ndugu Respitch Maengo na Katibu Tawala Msaidizi kitengo hicho kutoka Mkoa jirani wa Katavi Ndugu Sesemkwa.
 
Daktari wa Mifugo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Loomu akiwasilisha mada ya fursa za mifugo zinazopatikana Mkoani Rukwa. Zipo fursa nyingi Mkoani Rukwa ikiwemo mifugo mingi na ya aina tofauti yenye afya pamoja na wafugaji mahiri wadogo na wakubwa. ,Maeneo ya malisho, uwepo wa kiwanda cha kisasa cha nyama cha Saafi kinachomilikiwa na muwekezaji wa ndaji ni fursa nyingine.
 
Baadhi ya wadau wa Mkutano huo wakifuatilia mada tofauti ndani ya Ukumbi wa Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kikao hicho kitadumu kwa muda wa siku mbili ambapo maazimio mbalimbali yantegemewa kufikiwa kwa ajili ya kufanikisha adhma hiyo ya kuufanya Mkoa wa Rukwa eneo huru la magonjwa ya mifugo kuimarisha bishara ya mazao ya mifugo kimataifa.

JIONEE MAPOROMOKO YA MTO KALAMBO (KALAMBO FALLS) NA FUKWE ZA ZIWA TANGANYIKA MKOANI RUKWA

   

WIZARA YA KILIMO KUPITIA MRADI WA ASDP YATOA PIKIPIKI 8 KUSAIDIA UFUATILIAJI NA USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA KILIMO MKOANI RUKWA

Afisa Kilimo Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa Ndugu Oclan Chengula akikabidhi Pikipiki mbili kwa maafisa ugani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa miradi ya ASDP wilayani humo.
 
Pikipiki nyingine sita ambazo ziatatolewa kwa Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, na Wilaya ya Kalambo.

Wednesday, September 12, 2012

RAIS KIKWETE KATIKA ZIARA RASMI YA KISERIKALI YA SIKU TATU NCHINI KENYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya pamoja na ujumbe wake wakiingia Ikulu ya Nairobi Jumanne, 11 Septemba , 2012, alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya wakipata picha ya kumbukumbu Ikulu ya Nairobi Jumanne, 11 Septemba , 2012, alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya wakipata picha ya kumbukumbu Ikulu ya Nairobi Jumanne, 11 Septemba , 2012, alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mhe Bernard Membe na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Profesa Sam K. Ongeri
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na ujumbe wake na wenyeji wakiongea na wanahabari na kisha kupiga picha ya pamoja baada ya Mazungumzo yao Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya wakipongezana mara baada ya kuongea na waandishi wa habari
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mwai E. Kibaki wa Kenya wakipata picha ya kumbukumbu Ikulu ya Nairobi Jumanne, 11 Septemba , 2012, alipoanza Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu nchini humo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mhe Bernard Membe na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Profesa Sam K. Ongeri

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kulia kwake ni Waziri wa Elimu ya Juu, Mheshimiwa Margaret Kamar na kuhsoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Olive Mugendi.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi baada ya kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembezwa kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi baada ya kufungua rasmi Jengo la Shule ya Ukarimu na Utalii ya Chuo Kikuu cha Kenyatta.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea na kujionea shughuli mbalimbali za Taasisi ya Utatifi wa Kilimo ya Kenya (KARI)
 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na Rais Mwai E. Kibaki, Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga (kushoto) na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe Kalonzo Musyoka kabla ya Dhifa ya Kitaifa waliyoandaliwa na mwenyeji wao.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na ujumbe wake na wenyeji wao wakianza Mazungumzo Rasmi ya Kiserikali kati ya nchi hizo mbili.
 
Rais Mwai E. Kibaki akiongea wakati wa Dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika hoteli ya Inter Continental.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akijibu hotuba na baadaye kunyanyua glasi juu kuwatakia afya njema wenyeji wake wakati wa Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake katika hoteli ya Inter Continental.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akigonganisha glasi na Rais Mwai E. Kibaki wakati wa Dhifa ya Kitaifa katika hoteli ya Inter Continental. (Picha na State House)