Tuesday, October 30, 2012

INJINIA MANYANYA AJITOSA KUTETEA NAFASI YAKE YA UJUMBE WA NEC TAIFA KUPITIA JUMUIYA YA WAZAZI

Injinia Stella Martin Manyanya ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, MNEC Jumuiya ya Wazazi toka mwaka 2007, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Mjumbe wa SADC PF na Msimamizi wa Kimataifa wa Uchaguzi kupitia vionjo vya Uhandisi, Ujasiriamali na Sanaa alivyokuwa navyo ameamua kujitosa tena kwenye uchaguzi wa kutetea nafasi yake ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Jumuiya ya Wazazi katika uchaguzi utakaofanyika kesho tarehe 31/10/2012 Mkoani Dodoma. 
 
Vionjo vyake katika sanaa
 
Wasifu wake
 
Anaomba kura yako

Monday, October 22, 2012

MAZISHI YA PADRE WA KWANZA ALIYESOMEA SEMINARI YA KAENGESA JIMBO LA SUMBAWANGA‏ YAFANYIKA JANA


Askofu Damian Kyaluzi wa Jimbo katoliki la Sumbawanga akiendesha ibaada ya mazishi ya kumuombea marehemu Padre Augustino Kanyengere (75) hapo jana katika Kanisa kuu la Jimbo la Sumbawanga. Padre Kanyengere alifariki Oktoba 17 mwaka huu katika hospitali la Kristu Mfalme Mjini Sumbawanga kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu na kuzikwa hapo jana katika makaburi ya Katandala. Padre huyo ndiye aliyekuwa padre wa kwanza wa Kanisa hilo kupata Upadre kwa kutokea seminari ya Kaengesa inayomilikiwa na kanisa katoliki Jimbo la Sumbawanga iliyoanzishwa mwaka 1956. (Picha na Walter Mguluchuma - Sumbawanga)

Friday, October 19, 2012

WANANCHI WATEKETEZA MATREKTA KATIKA SHAMBA LA MALONJE LINALOMILIKIWA NA KANISA LA EPHATA MINISTRY MJINI SUMBAWANGA


Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.


Matrekta hayo yakiwa yameteketea kabisa kwa kuchomwa moto katika shamba hilo inalomilikiwa na kanisa la Efatha mkoani Rukwa.


Moja ya makambi yaliyoteketea kwa kuunguzwa na moto wakati wananchi hao
walipovamia mashamba hayo na kuchoma moto zana za kilimo katika shamba
hilo.
 

Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya Shamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba kwenye kambi hiyo.
 
Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara liyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo.
 
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa na kwamba wanatarajiwa kufikishwa wakati wowote mahakamani. (Picha na Joshua Mwakabungu-Sumbawanga)

WILAYA MPYA YA KALAMBO MKOANI RUKWA MSHINDI WA KWANZA WA SHUGHULI ZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2012 KANDA YA IV ILIYOSHINDANISHA MIKOA MITANO

Mkuu wa Wilaya mpya ya Kalambo Moshi Chang'a ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwenye shughuli za kuzima Mwenge wa Uhuru Mkoani Shinyanga akionyesha Kikombe na Cheti alichokabidhiwa na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama zawadi ya ushindi kwa Wilaya yake baada ya kushika nafasi ya kwanza katika shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012  katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake.
 
Hati kuithibitisha Wilaya ya Kalambo kutoka Mkoa wa Rukwa kuwa mshindi wa kwanza wa shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake.
 
 Wawakilishi wa Mkoa wa Rukwa waliokwenda kushiriki kuzima  mwenge wa uhuru Mkoani Shinyanga na kurudi na kikombe cha ushindi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a, mratibu wa Mwenge Kimkoa Abubakar Serungwe na Katibu wa Mkuu wa Mkoan Frank Mateny wakipewa mapokezi na uongozi na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa.
 
 Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akipokea kikombe hicho cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a muda mfupi baada ya kumpokea akitokea Mkoani Shinyanga alipokwenda kumuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwenye kilele cha kuzima mwenge wa uhuru.
 
 Watumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakifurahia kikombe hicho cha ushindi.
 
 Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ALhaj Salum Mohammed Chima akifurahia kikombe hicho kwa pamoja na watumishi wenzake.
 
 Hakika ushindi huo ulimgusa kila mmoja
 
 Ilifanyika tafrija fupi ya kupongezana kwa ushindi huo wa Wilaya ya Kalambo kwani umekuwa ni ushindi wa Mkoa mzima wa Rukwa kutokana na ushirikiano uliopo kutoka ngazi ya Mkoa hadi katika Halmashauri.
 
 Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa aikifurahia kikombe hicho.
 
 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akimpa Mkono wa pongezi Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a kwa ushindi alioupata wa Wilaya yake mpya kuwa mshindi wa kwanza wa shughuli za mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2012 katika kanda ya nne iliyohusisha Mikoa mitano ya Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa na Mbeya na Wilaya zake. Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chuma.

Thursday, October 18, 2012

BASI LA SUMRY LATEKWA LIKITOKEA SUMBAWANGA KWENDA MKOA JIRANI WA KATAVI


Moja ya mabasi ya kampuni ya Sumry likiwa tayari kuanza safari zake.
Watu wanane wenye silaha zikiwamo za jadi wameliteka basi la abiria la Sumry baada ya kuweka kizuizi cha magogo na mawe katika msitu wa Msaginya kijijini Magamba wilayani Mlele katika Mkoa wa Katavi katika barabara kuu ya Sumbawanga – Mpanda.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, uhalifu huo ulifanyika saa sita usiku wa kuamkia jana ambapo gari hilo lenye namba za usajili T107 BHT lililokuwa likisafiri kwenda mjini Mpanda likitokea mjini Sumbawanga.

Akifafanua, alisema basi hilo lilipofika eneo hilo lenye mteremko na kona kali ambalo lipo kilometa 15 kutoka Mpanda Mjini, lilikumbana na vizuizi vya mawe na magogo ndipo lilipolazimika kusimama ghafla.

Inadaiwa kuwa ndipo walipojitokeza watu wanane waliokuwa mafichoni wakiwa na silaha za jadi zikiwamo mapanga, nondo, mawe na visu na kuwalazimisha abiria wote kushuka ambapo walipekuliwa na kuporwa simu za mkononi 15 na kiwango kikubwa cha fedha, thamani halisi haijafahamika.

Kwa mujibu wa taarifa nyingine kutoka eneo hilo zinadai kuwa baadhi ya abiria walidhalilishwa kwa kuvuliwa nguo maungoni mwao wakati walipokuwa wakipekuliwa na watu hao ambao kila aliyeshuka garini, alilazimishwa kukabidhi chochote alichokuwa nacho kisha walilazimishwa kulala chini.

Kwa mujibu wa mtoa habari kutoka eneo la tukio ambaye hakuwa tayari jina lake liandikwe alisema baadhi ya abiria walikumbwa na adha hiyo walikuwa wanawake na watoto ambapo mmoja wao alikuwa mtawa wa kike ambaye inadaiwa alikuwa akisafiri kwenda Mwanza.
Hata hivyo, Kamanda huyo alikanusha abiria yeyote aliyevuliwa nguo ila walilazimishwa kulala chini baada ya kuamriwa kushuka garini na gari hilo baadaye liliwafikisha abiria wake hadi Mpanda Mjini.
Kwa mujibu wa Kidavashari kutokana na tafrani hiyo, watu wanane wakiwamo dereva wa gari, Said Chile na utingo wake ambaye jina lake halikufahamika mara moja walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya mjini Mpanda kwa matibabu.

Kamanda alisema Polisi inafanya msako mkali kuwasaka watu hao ambao hadi sasa hawajapatikana na haijulikani walikojificha kwani walikimbia kusikojulikana baada ya kufanya uhalifu huo. (Na Ziro99 blog)

 

WAFANYAKAZI OFISI YA MKUU WA WILAYA YA SUMBAWANGA KATIKA USAFI WA MAZINGIRA ALHAMIS YA KILA WIKI

Ikiwa kama ada ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kushiriki kwenye usafi wa mazingira katika kila siku ya alhamis ya kila wiki Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga ambayo pia ni sehem ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa imekuwa ikishiriki katika usafi huo kama inavyoonekana pichani ambapo Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ndugu Festo Chonya akiwaongoza wafanyakazi wenzake katika usafi huo. Hakika zoezi hili ni la kudumu katika mpango wa usafi aliouanzisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ujulikanao kama Sumbawanga Ng'ara.
 
Usafi huo haukuishia mazingira ya nje tu bali hadi ndani ya ofisi zao. Hapo dada Nazahedi Msangi na Deus Kaetano wakijumuika kwenye usafi huo. 
 
 Wafungwa wa kifungo mbadala (kifungo cha nje) nao walijumuika kwenye usafi huo.
 
Mzee Malingumu na Mama Kyamba wakishiriki kwenye usafi huo.

OMAN: RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI KUZINDUA UJENZI WA JENGO LA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI OMAN

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Oman katika mtaa wa balozi jijini Muscat Oman jana.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, (watatu kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ali Ahmed Saleh na (kulia) ni Afisa Mwandamizi Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, Bwana Abdallah Kilima.
 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua ujenzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Oman jana.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe,watatu kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Oman, Bw. Ali Ahmed Saleh, (wanne kulia aliyeshika karai) ni Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Oman, Bw. Abdallah Kilima na (kulia anayeshuhudia) ni Afisa katika Ubalozi huo, Bw. Saidi Mussa.Picha na Freddy Maro-IKULU.

Tuesday, October 16, 2012

KATIBU MKUU WIZARA YA ULINZI AONANA NA KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA KUZUNGUMZIA ZOEZI LA USAFIRISHAJI WA MAHINDI LINALOFANYWA NA JWTZ MKOANI HUMO

 Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Job Masima akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima Ofisini kwake leo alipomtembelea na wajumbe kutoka JWTZ Makao Makuu waliofika Mkoani Rukwa kwa ajili ya kujionea shughuli zinazoendelea kufanywa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo ni kuzoa shehena ya mahindi kutoka Mkoani Rukwa kwenda Mkoa jirani wa Katavi ambapo yatasafirishwa kwa reli kwenda Mikoa ya Kaskazini. Jumla ya tani 20,000 zinategemewa kusafirishwa na jeshi hilo ambapo mpaka sasa zimeshazolewa tani 11,000. Mahindi hayo yamenunuliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Chakula.
 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza na ugeni huo Ofisini kwake. Akizungumza katika kikao hicho Alhaj Chima alilishukuru jeshi hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya kwani mpaka sasa hakuna malalamiko yeyote yaliyojitokeza.
 
Baadhi ya maofisa wa jeshi hilo waliongozana na Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali  Watu Mkoa wa Rukwa Samson Mashalla.

Monday, October 15, 2012

BODABODA 200 WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI RUKWA

Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya akizungumza na vijana ambao ni madereva wa pikipiki maarufu kwa jina la boda boda juzi kwenye moja kituo cha bodaboda hizo alipowatembelea ili kujionea kama hali usafiri huo umerejea kama kawaida baada ya kutokea ukosefu nishati ya mafuta. Picha na Mussa Mwangoka.
--------------------------------
Mussa Mwangoka, Sumbawanga.

POLISI mkoani Rukwa, kupitia kitengo cha usalama barabarani kimesaidia vijana wapatao 200 ambao ni maderereva bodaboda kupata elimu ya sheria za usalama barabarani.

Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Rukwa, mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP), Boniface Mbao alisema hayo jana wakati wa kikao baina ya madereva bodaboda na mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mkoa huo (RDC).

Mrakibu huyo msaidizi wa Polisi, alisema jana kuwa kitengo cha usalama barabara kwa kushirikiana na chuo cha ufundi stadi cha Furaha Center kilichopo mjini Sumbawanga waliingia makubaliano ya kuhakikisha vijana hao wanapata elimu ya usalama barabara itakayowasaidia kuweza kumudu kuendesha vyombo vyao vya moto kwa kuzingiatia sheria.

"tuliona njia ya kuwasaidia si kuwakata kata hivyo tulizungumza na wenzetu wa chuo cha Furaha Center na tukakubaliana kuhusu vijana wa bodaboda kupata punguzo la ada ili waweze kujifunza sheria za barabarani, ambapo katika kipindi cha miezi 3 ada ilikuwa Sh 90,000 sasa imepunguzwa kwa vijana hao hadi kufika Sh 40,000 kwa miezi yote mitatu" alisema.

ASP Mbao mafunzo hayo ambayo yamewafikia vijana 200 kati ya madereva zaidi ya 300 yatawasaidia kupunguza ajali za boda boda ambazo ndizo idadi yake ni kubwa ukilinganisha na vyombo vingine vya moto, ambapo mara baada ya kumaliza mafunzo hayo, watakabidhiwa leseni.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya, alionya tabia ya baadhi ya waendesha bodaboda kuruhusu pikipiki zao kutumika kwa matukio ya uhalifu na kuwataka waache mara moja kwani watakaobainika sheria itachukua mkondo wake.

Pia Manyanya alisema kuwa wanapaswa kuheshimu kazi yao kwa kuwa wakiifanya vizuri ina kipato kikubwa kuliko kazi nyingine za maofisini ndio maana baadhi ya watu wenye elimu ya kuwawezesha kupata ajira Serikali na kwenye sekta binafsi wakiwamo walimu na wahasibu wamejikita kufanya biashara hiyo.