Wednesday, November 21, 2012

DKT. RAJAB RUTENGWE PAMOJA NA UKUU WA MKOA WA KATAVI NI MKULIMA WA MFANO NA WA KUIGWA

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Dkt. Rajab Rutengwe akitoa maelezo kadhaa kwa Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku mara baada ya kutembelea shamba lake la miembe lililoko katika kijiji cha Mboga mkoani Pwani.
……………………………………………
Nimesafiri na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe nikienda huko kwa mwaliko wa mkuu wa mkoa huyo kwa ajili ya shughuli maalum ya kumuvuzisha matukio katika uzinduzi rasmi wa mkoa huo utakaofanyika Novemba 25 mwaka huu mjini Mpanda ukizinduliwa na Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal.
Lakini tukiwa njiani tumepitia kwenye shamba la Mh. Dkt. Rajab Rutengwe lililoko huko Bagamoyo Mkoani Pwani katika kijiji cha Mboga mbele kidogo ya kijiji cha Msoga nyumbani kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete, Mh. Dkt. Rutengwe pamoja na majukumu yake ya uongozi katika mkoa wa katavi ni mkulima mzuri kwani shamba lake lina ukubwa wa hekari 15 na amepanda mazao mbalimbali yakiwemo Maembe, Mananasi, Mapapai Michungwa, mikorosho na pia anaendesha ufuganji wa nyuki na kuku jambo ambalo limekuwa mfano kwa wakazi wa kijiji hicho.
Mh. Dkt. Rutengwe anasema kwa kweli hawezi kununua kiwanja ambacho hakina eneo la kilimo kwani ukulima kwake ni jambo muhimu sana na ndiyo maana aliamua kuanzisha kilimo cha kisasa katika kijiji hicho kwa kupanda mazao mbalimbali kitu ambacho kimemfanya kuwa mkulima wa mfano katika kijiji chetu, endelea kuangalia matukio zaidi katika picha
Mh. Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe akizungumza na Meneja wa shamba lake Bwana Shamba Said Hemed wakati alipotembelea samba lake kuona maendeleo ya mazao katika shamba hilo.
 
Mh. Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe mmoja wa mti wa miembe ambayo imeshaanza kuzaa matunda shambani humo
 
Kama wageni shamabani hapo tulikaribishwa kupata tunda la Nanasi kidogo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi na mmiliki wa shamba hilo na kulia ni John Bukuku Mkurugenzi Mwendeshaji wa mtandao wa Fullshangweblog.
 
Meneja wa Shamba na hili Bwana Shamba Said Hemed akionyesha ukubwa wa shamba hilo lenye miembe zaidi ya Elfu nne.
 
Bw. Said Hemed akionyesma zao la matunda ya Mananasi katika shamba hilo.
 
Hili ni eneo ambalo limepandwa mipapai.
 
Hili ni moja wa mabada yameanza kujengwa kwa ajili ya ufugaji wa nyuki shambani hapo.
 
Hili ni moja ya mabanda ya kuku yanayojengwa katika shamba hilo kwa ajili ya ufugaji wa kuku wa kisasa wa mayai na nyama
 
Hili ni eneo lingine linaloandaliwa kwa ajili ya kupanda miembe mingine katika eneo hilo. (Picha kwa hisani ya fullshangweblog)

No comments:

Post a Comment