Sunday, November 25, 2012

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MKOA MPYA WA KATAVI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao ya Tanzania Dkt Mohamed Gharib Bilal na mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe wakizindua rasmi mkowa wa Katavi kwa kuweka jiwe la msingi katika kilima cha kijiji cha Kabungu kwa ajili ya kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya mkoa wa Katavi, Kijiji Cha Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka 1947 na Boma la mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo, baada ya uwekaji wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea mjini mpanda katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli mbalimbali za uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali zikiendana na sherehe za ngoma za makabila mbalimbali ya asili ya mkoa wa Katavi.
 
Makamuwa Rais Dkt. Gharib Bilal akikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Mh. Paza Mwamlima huku akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kijijini hapo.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabungu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua mkoa wa Katavi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kutoka kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Bw. Mselem Said.
 
Mkuu wa mkoa wa Katavi akimkaribisha Makamu wa Rais Dt. Gharib Bilal ili kuongea na wananchi wa kijiji cha Kabungu.

Msafara wa magari ya Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal ukiwasili katika eneo lilipowekwa jiwe la msingi kwa uzinduzi wa mkoa wa Katavi katika kilima cha kijiji cha Kabungu Mkoani Katavi.
 
Wazee waasisi wa kijiji cha Kabungu wakinyanyua matawi ya miti juu kama ishara ya kumpokea Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal wakati alipowasili katika kijiji hicho leo.

Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakiimba wimbo mara baada ya Makamu wa Rais kuwasili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda tayari kwa Sherehe za kuzindua mkoa wa Katavi
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa mkoa wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili kulia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt. Mary Nagu.
 
Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe, Naibu Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya wakiwa katika sherehe za uzinduzi huo.
 
Baadhi ya wawekezaji waliohudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili.
 
Mkuu wa mkoa wa Katavi akiongea na kukaribisha viongozi mbalimbali kutoka salam zao kutoka mikoa waliyotoka na wizara mbalimbali.
 
Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye akizungumza na wana Katavi na kuwaasa mambo mbalimbali kuhusu ardhi yao hasa katika suala zima la uwekezaji, ambapo amewaambia wasiuze ardhi bali waingie ubia na wawekezaji ili kunufaisha vizazi vyao pia.

Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwasalimia wananchi wa Katavi na kuwapongeza kwa kupata mkoa mpya wa Katavi.
 
Mama Aisha Bilal akisalimia wananchi wa katavi katika sherehe hizo.
 
Kwaya ya Vijana ya Moravian mjini Mpanda wakitumbuiza katika uzinduai huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda.
 
Martha Mbogo mwimbaji wa kundi la Katavi Curture Group akiimba wakati kundi hilo lilipokuwa likitumbuiza katika uzinduzi huo mjini Mpanda.
 
Wananchi wa Mpandawakinyanyua mkono yao juu kama ishara ya kushangilia kuazinduliwa kwa mkoa wao wa Katavi uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.
 
Wananchi wakiwa wanashangilia
 
Watoto Daniel Ntwangile na Christina Benadito wakitunzwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuimba na kucheza vizuri na Kwaya ya Vijana Moravian Mjini Mpanda wanaofuatia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakijiandaa na wao kuwatunza
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Veta Chuo cha Veta Mpanda Trojemsi Bashato wakati alipotembelea banda la Veta.

Makamu wa Rais akisikiliza maelezo kutoka kwa Thomas Lemunge mfanyakazi wa kampuni ya simu ya TTCL wakati alipotembelea Banda la kampuni hiyo, kulia ni Bw Huphrey Ngowi mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa huduma Mwandamizi wa benki ya Wanawake TWB BiMargaret Msengi wakati alipotembelea katika banda hilo leo.
 

Makamu wa Rais Akizungumza na wafanyakazi wa benki ya NMB wakati alipotembelea katika banda hilo leo njini Mpanda Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe.
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wana Katavi wakati wa uzinduzi wa mkoa wa mpya wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wana Katavi wakati wa uzinduzi wa mkoa wa mpya wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo. PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM.

No comments:

Post a Comment