Friday, November 23, 2012

WAZIRI MKUU PINDA AWASILI MKOANI KATAVI KWA SHUGHULI ZA UZINDUZI WA MKOA HUU MPYA, ATEMBELEA MABANDA YA MAONESHO

 Ndege iliyokuwa imembeba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Mpanda mapema hii leo. Waziri Mkuu atakuwa Wilayani Mpanda kwa shughuli kuu mbili ambayo moja ni kikao cha tathmini ya kongamano la uwekezaji lililofanyika wilayani hapa Oktoba mwaka jana pamoja na uzinduzi wa Mkoa mpya wa Katavi ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mhe. Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal na kilele itakuwa siku ya jumapili tarehe 25/11/2012.
 
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Dkt. Rajab Rutengwe mara baada ya kuwaisili katika uwanja wa ndege wa Mjini Mpanda mapema hivi leo.
 
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Col. Mst. Issa Machibya mara baada ya kuwaisili katika uwanja wa ndege wa Mjini Mpanda mapema hivi leo.
 
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda aikipokea maelezo kuhusu uwekezaji kutoka kwa Muwezeshaji katika banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Bwana Misasi Nyanda Marco ambaye pia ni Afisa katika dawati la uwekezaji.

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniia Mhe. Mizengo Kayanza Pinda (kulia), Mama Tunu Pinda (Katikati), Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe na washiriki wengine walihudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Mkoa mpya wa Katavi wakimsikiliza kwa makini muwezeshaji (Hayupo pichani) katika banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa. 
 
 Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Mhandisi Emmanuel Kalobelo akifurahia jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mhe. Marry Nagu wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Pinda leo katika uwanja wa ndege wa mjini Mpanda.
 
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mhe. Iddi Hassan Kimanta akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Mhe. Marry Nagu mapema leo asubuhi kwenye mapokezi ya Mhe. Waziri Mkuu katika uwanja wa ndege wa Wilayani Mpanda.
 
 Wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii  PSPF Mkoa wa Rukwa, Kulia ni Afsa Mfawaidhi wa Mfuko huo kwa Mkoa wa Rukwa ndugu Ileth Mawala na mfanyakazi mwenzake wa Mfuko huo ndugu Paul Mbijima wakiwa kwenye banda la PSPF kunadi sera za mfuko kwa wananchi mbalimbali na wawekezaji wanaotembelea mabanda ya maonesho katika ukumbi wa idara ya maji mjini Mpanda. 
 
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Mtandao wa kijamii wa fullshangweblog.com Bwana John Bukuku wakati wa maandalizi ya mapokezi ya Mhe. Waziri Mkuu katika uwanja wa ndege wa Mpanda.

 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Col. Mst. Issa Machibya akizungumza na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa bwana Hamza Temba ambaye pia Muendeshaji wa mtandao wa Ofisi hiyo wa rukwareview.blogspot.com katika uwanja wa ndege wa Mpanda wakati wa mapokezi wa  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda.


Muwezeshaji katika banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Bwana Misasi Nyanda Marco ambaye pia ni Afisa katika dawati la uwekezaji akitoa maelezo juu ya fursa zinazopatikana Mkoani Rukwa kwa watu mbalimbali waliokuwa wakifurika katika banda hilo.
 
Wawezeshaji katika banda la Rukwa wakinadi sera kwa wananchi waliofika katika banda hilo, Kulia ni Catherine Peter kutoka idara ya Afya Mkoa, James Kapenulo Afisa Takwimu Mkoa na Lydia Kipeta kutoka Idara ya Afya Mkoa wa Rukwa.


No comments:

Post a Comment