Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akisoma hotuba ya ufunguzi wa kikao cha uhamasishaji wa mkakati wa mawasiliano ya mabadiliko ya tabia katika kupambana na Malaria kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa mkutano wa Libori Centre wilayani Sumbawanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Dkt. Yahya Hussein akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kufungua kikao hicho.
Mwenyekiti wa asasi ya RODI akitoa maelezo mafupi na madhumuni ya kikao hicho mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na washiriki wa kikao hicho.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa na Katavi,
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Katavi
Wataalamu na Watendaji kutoka Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii,
Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa na Katavi,
Wawezeshaji wa Warsha hii,
Waganga Wakuu na Waratibu wa Malaria,
Wataalamu na Watendaji kutoka Hospitali ya Mkoa.
Watendaji kutoka Sekretarieti ya Mkoa,
Watendaji kutoka Halmshauri za Mkoa wa Rukwa na
Katavi,
Ndugu Waandishi wa Habari,
Mabibi
na Mabwana.
Asalam
alykum, Bwana Yesu asifiwe, tumsifu Yesu Kristo.
Awali
ya yote napenda kuchukua fursa hii kwa namna ya pekee kumshukuru Mwenyezi Mungu
mwingi wa Rehema kwa kutukutanisha Siku hii ya leo.
Aidha
napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kuwasafirisha salama wale wote
ambao wanatoka nje ya Manispaa yetu ya Sumbawanga poleni kwa safari ndefu na karibuni sana, Manispaa
yetu ya Sumbawanga hali ni shwari na tulivu Usalama umeimarishwa. Huduma zote
za Msingi zipo mtafurahia uwepo wenu Mkoani Rukwa.
Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha
wageni wetu kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na taasisi isiyo ya
kiserikali ya Johns Hopkins University – (Center for Communication Programs) kwa
kututembelea na kutoa mwanya wa kuwa na majadiliano ya pamoja namna ya
kuukabiliana na ugonjwa wa malaria katika
Mkoa wa Rukwa na Mkoa wa Katavi.
Napenda kuipongeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Wadau na Wafadhili mbalimbali kwa
jitihada zinazofanywa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria nchini.
Mradi wa Communication and Malaria Initiative in
Tanzania (COMMIT) unaotekelezwa na Johns Hopkins University Tanzania (JHU) unalenga
kuleta mabadiliko ya tabia kwa wanajamii dhidi ya Malaria nchini Tanzania.
Mradi umetekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano(5) lakini kwa Rukwa na Katavi
umetekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili.
Mradi huu unatekelezwa kwa kutumia mawakala wa
kusaidia kubadilisha tabia ndani ya jamii katika Kata za mradi ambao hujulikana
kwa majina ya CCA (Community Change Agent).
Mafanikio mazuri kwa jamii katika kutumia
mawasilianao yanayolenga kubadilisha tabia na kutoa elimu mbalimbali Kama;
·
Matumizi sahihi ya vyandarua vyenye Viuatilifu kila siku kwa mwaka
mzima.
·
Hati punguzo kwa Wajawazito.
·
Kuhudhuria Kliniki mapema kwa wajawazito.
·
Dawa ya kinga ya Malaria kwa wajawazito.
·
Matumizi sahihi ya Dawa ya mseto
ya Malaria.
·
Kuwahi vituo vya huduma mtu anapojihisi kuwa na dalili za malaria.
Elimu hii imekuwa ikitolewa kwa njia mbalimbali
kwenye mikusanyiko ya watu kama vile kwenye Masoko, Shule, Vituo vya Afya na
sehemu nyingine. Pia kwa mtu mmoja mmoja kupitia nyumba kwa nyumba.
Hadi mradi
unamaliza muda wake Johns Hopkins University (JHU) waliona ni vyema kuwe na
mikakati ambayo itasaidia mradi endelevu ndani ya jamii. Hivyo, JHU imefanikiwa
kupata fedha za kuendesha mradi kwa kipindi
cha mwaka mmoja. Wameamua kwa awamu hii washirikiane
na jamii na Serikali kusimamia huduma hii ambayo imeonyesha mafanikio mazuri
ndani ya jamii kwa kipindi chote cha maisha yake.
Johns Hopkins University (JHU) kwa kushirikiana na RODI,
imeandaa semina hii inayoshirikisha wadau mbalimbali muhimu katika kufikia lengo
lililokusudiwa. Michango yetu ni muhimu sana ndani ya Idara na jamii, hivyo
tushirikiane kwa pamoja tuone tunafanyeje na ni mikakati ipi inayoweza kusaidia
kuleta mabadiliko ya kitabia katika jamii.
Pamoja na mikakati iliyopangwa kuendeshwa na Johns
Hopkins University CCP TZ katika mradi wa COMMIT kwa kipindi hiki cha mwaka
mmoja mkoani Rukwa na KATAVI ni kuona kwamba JHU kama taasisi isiyo ya kiserikali
inatoa mchango wake katika jamii. Pia ofisi ya RAS/DED kupitia Halmashauri
ndani ya ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya kunakuwepo bajeti kwa ajili ya CCA (Community
Change Agent) ya kuendesha mapambano dhidi ya Malaria kupitia mabadiliko ya
tabia ndani ya Wilaya husika mara baada ya mradi huu wa COMMIT kuisha.
Nimatumaini yetu sisi kama wadau, Wote kwa pamoja tutapanga mikakati itakayotoa dira
nzuri inayoshirikisha wadau wote muhimu katika mapambano dhidi ya malaria mkoani Rukwa.
Ndani ya warsha hii wanashiriki watalamu kutoka
sekta ya Afya ,Maafisa mipango, Taasi binafsi ‘CBO’s zinazoshiriki katika mradi
huu ili kwa pamoja tusaidiane kupanga
mipango itakayoleta tija nzuri ya mabadiliko ya kitabia ndani ya jamii. Pamoja
na kujadili mipango endelevu ya shughuli za malaria pia warsha hii itatoa
mwanya wa kujadili maada kuhusu uongozi na mipango.
Pamoja na taarifa hizo zinazoashiria mradi kuwa na
mafanikio makubwa, ni vema sasa taarifa kamili zitakazoeleza mafanikio hayo
ziwe kwa undani zikielezea mafanikio katika ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa ili
matokeo ya mradi yaweze kupimika vizuri zaidi.
Mwisho nawatakia
majadiliano mema na yenye tija ninawataka mshiriki kikamilifu katika kuibua
mkakati wa kupambana na Malaria. Ili Mkakati huo uweze kuwa rahisi kutekelezwa
na Wadau wote pia mnajukumu la kuhakikisha elimu inatolewa katika maeneo yenu
ya kazi kwa kuwa na vikao vya kuelimisha
watendaji, waheshimiwa madiwani na Wananchi kwa ujumla.
Vilevile mkakati huo uwasilishwe
kwenye vikao halali vya Halmashauri,(CCHP) ili sisi wote tuwe washiriki katika
kazi ya kuelimisha na kuhamasisha Wananchi kuupokea na kutekeleza mradi huu.
Nashukuru kwa kunisikiliza.
MABADILIKO YA KITABIA
YANAWEZEKANA, TUSHIRIKIANE KUTOKOMEZA MALARIA.
Natamka kuwa Warsha
hii imefunguliwa rasmi
Eng.
Stella Martin Manyanya(Mb)
MKUU
WA MKOA WA RUKWA
Post a Comment