Friday, December 14, 2012

UJENZI WA BARABARA YA SUMBAWANGA-MATAI-KASANGA KWA KIWANGO CHA LAMI

Barabara hii ya Sumbawanga-Matai-Kasanga (112 KM) inajegwa na Kampuni ya China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G)/ Newcentry Company Ltd. chini ya Mhandisi Mshauri Nicholas O’Dwyer and Company Limited kutoka Ireland akishirikiana na Apex Engineering Ltd, kutoka Tanzania. Gharama ya Mradi ni Sh. 133.30 bilioni.
Maendeleo ya jumla ya mradi hadi kufika tarehe 31 Octoba, 2012 yalikuwa 28% ya kazi zote zilizopangwa. Mradi huu unatekelezwa kwa mkataba wa Usanifu na Ujenzi (Design and Build Contract). Kwa sasa kazi zinaendelea vizuri baada ya kusuasua siku za nyuma. Mradi huu ulitegemewa kukamilika tarehe 13 Januari, 2013 lakini itabidi muda wa utekelezaji kuongezeka kutokana sababu mbalimbali.
 
Lami imeanza kumiminwa katika barabara hii, Pongezi kwa Serikali ya awamu ya nne inyoongozwa na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwani katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru Mkoa wa Rukwa ulikuwa bado haujaunganishwa kwa lami na Mikoa mingine ya jirani, Kwasasa jumla ya miradi mikubwa sita ya kuunganisha Mkoa wa Rukwa na Mikoa jirani ya Mbeya na Katavi pamoja na Wialaya zake za Kalambo na Nkasi inaendelea.

No comments:

Post a Comment