Wednesday, December 5, 2012

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI MKOANI RUKWA

Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt Charles  Tizeba(aliyevaa suti ya kaki), akisisitiza jambo kwa Uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), alipotembelea Bandari ya Kasanga Mkoani Sumbawanga jana asubuhi.
 
Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Sebastian Nandi akimuonyesha eneo la Bandari ya Kasanga, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba(aliyevaa suti ya kaki), jana. Naibu Waziri wa Uchukuzi yuko Mkoani Rukwa kwa ziara ya kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi.
 
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt Charles Tizeba (aliyevaa suti ya kaki ),akiangalia maporomoko ya Kalambo yaliyoko Mkoani Rukwa jana. Maporomoko hayo ni ya pili kwa ukubwa barani Afrika, ya kwanza yakiwa yale ya Viktoria Falls yaliyoko Zimbabwe.
 
  Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt Charles  Tizeba(aliyevaa suti ya kaki), akisisitiza jambo kwa Uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), alipotembelea Bandari ya Kasanga Mkoani Sumbawanga jana.
 
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt Charles Tizeba(aliyevaa suti ya kaki),akifafanua jambo kwa uongozi wa kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga katika ofisi za kiwanja hicho jana.

  Muonekano wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga. Kwa mwaka 2012 idadi ya abiria imefikia wastani wa 200 kwa Mwezi ikilinganishwa na miaka ilipita na matarajio kufikia mwishoni mwa mwaka 2012 idadi ya abiria itazidi na kufikia 1,000.
  Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi na Ufundi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege(TAA), Mhandisi George Sambali, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba(aliyevaa suti ya kaki),ya namna ambavyo Uwanja wa Ndege Mpya Unaotaka kujengwa katika eneo la Kisumba mkoani Sumbawanga utakavyokuwa jana. (Picha na Lisso Biseko-Afisa Habari Wizara ya Uchukuzi)

No comments:

Post a Comment